24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TANCDA: Marufuku ya shisha yataokoa afya za vijana wengi

Shisha1Na Hamisa Maganga, Dar es Salaam

SIKU zote wanaovuta sigara hadharani, huwaathiri zaidi watu wa pembeni ambao huvuta ule moshi kutoka kwa mvutaji.

Hii imekuwa ikichangia magonjwa kadhaa yasiyo ya kuambukiza kwa jamii, ambayo kwa kawaida hayasambazwi na mgonjwa kwenda kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo.

Akizungumza na mwandishi wa makala haya, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA), Dk. Tatizo Waane, anasema kuwa chanzo cha magonjwa yasiyo ya kuambikiza ni mitindo ya maisha ya watu ikiwamo uvutaji wa shisha.

Anayataja maradhi hayo kuwa ni pamoja na moyo na mishipa ya damu, figo, saratani, kifua sugu, kisukari, magonjwa ya akili na mengine ya kurithi kama selimundu.

Kwa sababu hiyo, TNCDA wanaipongeza Serikali kwa kutoa amri ya kuzuia matumizi ya shisha nchini.

Anasema matumizi ya tumbaku yanahusishwa na saratani za mapafu na koo, vidonda vya tumbo, kifua sugu na magonjwa mengine mengi.

“Tunaipongeza Serikali kwa kupiga marufuku uvutaji holela wa sigara pamoja na matumizi ya shisha, iliyokuwa ikiangamiza afya za vijana wengi hapa nchini na kusababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza,” anasema Dk.Waane.

Anasema TANCDA wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha Watanzania wanaepuka magonjwa haya kwa kuzingatia kanuni za afya ikiwamo kutotumia shisha na tumbaku.

Anabainisha kuwa mwaka 1999, magonjwa yasiyo ya kuambukiza yalikadiriwa kuchangia karibu asilimia 60 ya vifo vyote duniani na asilimia 43 ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani. “Tatizo hili linakua kwa kasi katika nchi zinazoendelea, Tanzania ni miongoni…

inakisiwa kuwa mwaka 2020 magonjwa haya yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na asilimia 60 ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani.

Julai 5 mwaka huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipiga marufuku matumizi ya shisha kwa kuwa huwafanya vijana washindwe kufanya shughuli za uzalishaji mali hivyo Serikali kukosa nguvu kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles