MOSCOW, Urusi
SERIKALI ya Urusi imezitaka nchi zilizo karibu na Afghanistan kutokubali kupokea vikosi vya kijeshi vya Marekani na Umoja wa Kujihami wa Ulaya (NATO).
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov, wanajeshi wa pande mbili hizo hawapaswi kuingia tena Afghanistan kwani walishaondoka nchini humo miezi michache iliyopita.
Kile kilichoelezwa na vyombo vya habari vya Iran ni kwamba Levron aliyasema hayo katika mkutano uliowakutanisha mawaziri wa mambo ya nje wa Iran, Pakistan, Turkmenistan, Tajikistan na Uzbekistan, ambapo yeye na mwenzake wa China walishiriki kupitia teknolojia ya video.
“Tunaziomba zilizoko jirani na Afghanistan kutoruhusu uwepo wa majeshi ya Marekani na NATO, ambayo yamepanga kwenda pale baada ya kuondoka,” amesema Lavrov.