27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Tuchel: Chelsea nileteeni Icardi

LONDON, England

MKUU wa benchi la ufundi la Chelsea, Thomas Tuchel, amewaambia mabosi wa klabu hiyo kumrahisishia kazi kwa kumsajili mshambuliaji aliyekuwa naye PSG, Mauro Icardi.

Tuchel anamtaka Icardi, licha ya kwamba tayari kikosi chake kina Romelu Lukaku, Timo Werner na Kai Havertz wanaocheza eneo hilo la upachikaji mabao.

Kwa msimu mmoja aliocheza chini ya Tuchel, Icardi raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 28, alichangia mabao 20 katika mechi 34 za mashindano mbalimbali.

Licha ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha PSG, bado zimekuwapo taarifa zinazodai Icardi atafungasha kila kilicho chake endapo klabu hiyo itapokea ofa ya kueleweka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles