27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

KMC kusaka ushindi wa kwanza kwa Kagera Sugar

Na MWANDISHI WETU

BAADA ya kukosa ushindi katika michezo yake minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kikosi cha KMC kesho Oktoba 29,2021 kinatarajia kushuka dimbani kuivaa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Timu hiyo inahitaji kupata ushindi ili kurudisha Imani kwa mashabiki wake kutokana na mwenendo walionza nao wa kukosa matokeo ya ushindi.

Katika michezo hiyo, KMC ilifungwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania, ikatoka suluhu na Coastal Union, ikafungwa na Yanga 2-0, kisha kutoka sare ya 1-1 na Namungo FC, hivyo kukaa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala, amesema kesho wanaanza mechi wakiwa nyumbani na watahakikisha ushindi unapatikana ili kurejesha heshima yao.

Amesema wanafahamu ugumu wa mchezo huo, lakini benchi la ufundi limefanya maandalizi ya kutosha na kurekebisha makosa yaliyojitokeza mechi  zilizopita.

“ Licha ya kuwa hatuna matokeo mazuri, lakini mashabiki wetu bado wanaendelea kuwa pamoja na sisi hivyo tuna deni kubwa kwao la kuhakikisha tunawapa burudani yenye matokeo mazuri kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya wapinzani wetu Kagera Sugar,”amesema Christina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles