31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

URUSI YAPIGANIA KUACHIWA KWA KIGOGO WAKE UFARANSA

SOCHI, URUSI


SERIKALI ya Urusi imesema itafanya kila liwezekanalo ili kulinda masilahi ya kisheria ya seneta wake, Suleiman Kerimov, ambaye anashikiliwa nchini Ufaransa.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, aliwaambia wanahabari mjini hapa jana kuwa seneta huyo kama walivyo raia wengine wa nchi hii, Serikali ina dhamana ya kuhakikisha inamlinda kisheria.

“Kwa jinsi hali ilivyo na kiukweli, Kerimov ni raia wa Urusi kama walivyo raia wengine, hivyo tuna dhamana ya kufanya  jitihada ili kulinda masilahi yake kisheria,” alisema Peskov.

Alisema miongoni mwa jitihada zinazofanywa na Serikali ni kwamba tayari mjumbe ameshatumwa nchini Ufaransa ili kushughulikia suala hili.

“Ni muhimu kuona Suleiman Kerimov ndiye mmiliki wa pasipoti ya kidiplomasia, ambayo aliingia nayo Ufaransa. Ndiyo sababu tunafanya kazi kubwa ya kulinda masilahi yake,” aliongeza msemaji huyo.

Seneta Kerimov ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la Seneta nchini hapa, alikamatwa mwanzoni mwa wiki akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Nice kisha akapelekwa kituo cha polisi.

Shirika la Habari la Reuters, liliripoti mapema juzi kuwa waendesha mashtaka wa Ufaransa wanamshikilia seneta huyo kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles