23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

IMF YAIONYA KENYA KUHUSU DENI

NAIROBI, KENYA


SHIRIKA la Fedha Duniani (IMF) limeionya Kenya juu ya ukubwa wa deni linaloendelea kuongezeka, kuwa linahitaji kudhibitiwa ili kuzuia kuathiri vibaya uchumi wa taifa hilo siku za usoni.

Mwakilishi wa IMF nchini Kenya, Jan Mikkelsen, alisema pamoja na kwamba uchumi wa Kenya umeonekana kuwa thabiti licha ya siasa na ukame, deni linaloendelea kuongezeka linaweza kuyumbisha uchumi katika siku zijazo.

Deni la Kenya limeendelea kuongezeka kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kutoka chini ya Sh trilioni moja ya Kenya mwaka 2014 hadi Sh trilioni 4.4 Septemba 2017.

Kulingana na mwakilishi huyo, Kenya inahitaji sera wazi kukabiliana na tishio la deni.

IMF ilitoa tahadhari hiyo, huku Serikali ikiwa imepanga kupata mkopo shirikishi na hati ya ukopeshaji ya Eurobond kwa awamu ya pili.

“Deni linahitaji kupunguzwa ili kutoa nafasi zaidi kwa sekta ya binafsi na kudhibiti shinikizo kwa umma,” alisema mkurugenzi huyo wakati wa mahojiano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles