29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Upinzani DRC wakataa mazungumzo ya AU

Edem Kodjo
Edem Kodjo

KINSHASA, DRC

MUUNGANO mpya wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umekataa jaribio la mwisho la Umoja wa Afrika (AU) kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kuleta utulivu wa kisiasa nchini hapa.

Katika taarifa yake iliyotolewa baada ya mkutano wa dharura, upinzani umemshutumu mpatanishi wa AU, Edem Kodjo kuonesha upendeleo wa dhahiri.

Lilisema Kodjo anataka kuhakikisha Rais wa sasa Joseph Kabila anawania muhula wa tatu wa urais kinyume na katiba ya taifa hilo.

Kundi hilo sasa limeitisha mgomo mkubwa kesho, ambayo Kodjo, waziri mkuu wa zamani wa Togo alitaka kufanyika mazungumzo hayo baada ya serikali kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa.

Upinzani unataka Kabila ahitimishe utawala wa miaka 15 Desemba mwaka huu kwa mujibu wa Katiba, lakini mamlaka zinasema uchaguzi hauwezi kufanyika Novemba mwaka huu kama ilivyopangwa.

Aidha Mahakama Kuu ilisema Rais Kabila atabakia madarakani hadi uchaguzi utakapofanyika.

Hiyo ilitokana na kazi ya uandikishaji wapiga kura kutangazwa na tume ya uchaguzi kuwa haitakamilika kwa wakati kabla ya uchaguzi huo bali hadi Julai 2017.

Zoezi la kusajiri wapiga kura zaidi ya milioni  30 lilianza Machi mwaka huu na litachukua miezi 16 kukamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles