Mtoto aua watu 51 harusini Uturuki

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

ISTANBUL, UTURUKI

MTOTO mwenye umri wa miaka kati ya 12 na 14 amejitoa mhanga na kuua watu 51 katika jiji la Gaziantep nchini hapa, Rais, Recep Tayyip Erdogan, amesema.

Erdogan alisema kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS) lilikuwa nyuma ya shambulio hilo la juzi, ambalo lililenga harusi ya Wakurd.

Kwa mujibu wa Rais Erdogan, bomu hilo lilijeruhi watu 69, wakiwamo 17 walio mahututi.

Ameongeza kwa kusema hakuna tofauti kati ya IS, vuguvugu lililopigwa marufuku la PKK na wafuasi wa kiongozi wa kidini aliyeko uhamishoni nchini Marekani Fetullah Gulen, ambaye analaumiwa kupanga jaribio la mapinduzi lililotibuka mwezi uliopita.

Gaziantep, uliopo karibu na mpaka na Syria unajulikana uwapo wa kambi kadhaa za IS.

Jiji hilo lenye wakazi milioni 5.1 limekuwa likikumbwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kujitoa mhanga na milipuko ya mabomu kutokana na vita inayoendelea Syria pamoja na wanamgambo wa Kurd.

Gavana wa jimbo hilo, Ali Yer-likaya, ametaja shambulio hilo kama tukio la kigaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here