26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

UPELELEZI KESI YA MPEMBA UMEKAMILIKA

unnamed-4a

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam

UPANDE wa Jamhuri umedai mahakamani kwamba upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Yusuf Ali Yusuf (Mpemba) na wenzake watano umekamilika, na jalada liko kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO) na litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hayo yalidaiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipotajwa baada ya Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde kueleza upelelezi umekamilika.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita kwa upande wake alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika kwa hatua za awali, jalada lipo kwa ZCO na baadaye litapelekwa kwa DPP kwa ajili ya hatua zaidi.

Wakili Nehemia Nkoko anayemtetea Mpemba, alihoji upande wa Jamhuri mara ya mwisho ulidai taratibu zinafanyika washtakiwa waweze kusomewa maelezo ya awali ili kesi iweze kuhamishiwa katika mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza ama kitolewe kibali cha kuruhusu isikilizwe Mahakama ya Kisutu.

Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kutoa majibu sahihi Desemba 29, 2016.

Mbali na Mpemba, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo, ni Charles Mrutu maarufu kama Mangi Mapikipiki ama Mangi Mpare, Benedict Vintus Kungwa, Jumanne Ramadhan Chima maarufu kama Jizzo ama JK, Ahmed Ambari Nyagongo na Pius Vicent Kulagwa.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne ya uhujumu uchumi, likiwamo la kujihusisha na mtandao wa uhalifu na kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh 785.

Katika kesi hiyo, wanadaiwa kati ya Januari 2014 na Oktoba 2016 katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Tanga na Mtwara kwa pamoja walijihusisha na mtandao wa uhalifu kwa makusudi.

Washtakiwa hao, wanadaiwa kuendeleza malengo ya mtandao wa kukusanya na kuuza vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh 392,817,600 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Oktoba 26, 2016 huko Mbagala Zakhem, Wilaya ya Temeke, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa walikamatwa wakiwa na vipande 10 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 13.85 vyenye thamani ya Sh 65,469,600 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Oktoba 27, 2016  huko Tabata Kisukulu wilaya ya Ilala washtakiwa hao wanadaiwa walikamatwa wakiwa na vipande 4 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 11.1 vyenye thamani ya Sh 32,734,800 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Washtakiwa hao, pia wanadaiwa kuwa Oktoba 29, 2016 huko Tabata Kisukulu wilayani Ilala, walikamatwa wakiwa na vipande 36 vya meno ya tembo yenye uzito wa kilogramu 58.55 na thamani ya Sh 294,613,200 mali ya Jamhuri ya Muungano bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles