28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

KINANA ATOA MWEZI MMOJA MALI ZA CCM KUHAKIKIWA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.

Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, kuhakikisha wanahakiki mali zote zinazomilikiwa na chama hicho.

Kinana aliyasema hayo jana, wakati ya uzinduzi wa jengo la ghorofa nane lililogharimu Sh bilioni 7, lililopo Kibasila, Upanga, Dar es Salaam, ambalo watapangishwa watu mbalimbali.

Alisema moja ya agenda kuu iliyojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama hicho Desemba 13, mwaka huu, ilikuwa ni pamoja na uhakiki wa mali za chama nchi nzima.

“Tulipokea uhakiki wa kila mkoa kwa lengo la kuzijua na zinakinufaisha nini chama, tunafanya kazi ya kuzichambua.

“Dar es Salaam inaongoza kuwa na mali nyingi zinazohamishika na zisizohamishika, natoa mwezi mmoja  kwa viongozi kuhakiki mali na kujiridhisha kama zinasaidia chama,” alisema Kinana.

Alisema baada ya muda huo, atafanya ziara ya kutembelea mali hizo katika baadhi ya maeneo yaliyopo wilaya zote kwani anataka mali zote ziwe mikononi mwa chama hicho.

Kinana alisema baada ya ziara ya Dar es Salaam, atatembelea mikoa mingine 13 ambayo inaongoza kwa kuwa na mali za chama hicho.

Katika hatua nyingine, Kinana alizungumzia sababu za chama hicho kupunguza baadhi ya wajumbe waliokuwa wakishiriki mikutano ya Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, kuwa ni kupunguza urasimu miongoni mwa baadhi ya viongozi.

“Kikao cha juzi kilikuwa kikao cha historia, kilikuwa cha kwanza kwa Mwenyekiti wa chama, Rais Dk. John Magufuli, kimefanya mambo makubwa kwa masilahi ya kila mwanachama.

“Tuliamua kupunguza idadi ya wajumbe kwa sababu ya kuondoa urasimu, kutoka 388 hadi 158, kwa sababu ni kikao cha uwakilishi hakuna haja ya kuwa wajumbe wengi,” alisema Kinana.

Habari hii imeandaliwa na PATRICIA KIMELEMETA, JONHANES RESPICHIUS Na ATUPENDA GEOFREY (MPS)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles