29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

UPELELEZI KESI YA KUBAKA WANAFUNZI WAKAMILIKA

criminal-law

NA MANENO SELANYIKA-DAR ES SALAAM

UPELELEZI wa kesi ya kubaka na udhalilishaji inayowakabili wanafunzi tisa kutoka Shule ya St. Maria, Salome iliyopo Boko Jijini Dar es Salaam umekamilika.

Wanafunzi hao wenye umri kati ya miaka 15 na 21wanatuhumiwa kwa kosa la kumbaka na kumtomasa mwezao (jina limehifadhiwa) wakati walipokuwa katika maeneo ya shule hiyo.

Shauri hilo lilitajwa jana mbele ya Hakimu Iz- Haq Kuppa, Wakili wa Serikali Joseph Nasua, alidai mahakamani hapo kwamba shtaka hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi umekamilika hivyo kuomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na Wakili Nasua ilidaiwa kwamba shtaka la kwanza la kubaka linalomkabili mtuhumiwa wa kwanza Frank Misokia (18), alifanya kitendo hicho kiovu Novemba 4 mwaka huu shuleni hapo.

Shtaka la pili linawakabili watuhumiwa waliobakia ambapo kwa mujibu wa maelezo ya shtaka hilo watuhumiwa wanakabiliwa na kosa la kupenyeza vidole sehemu za siri za msichana huyo wakati wakitambua ni kinyume cha sheria.

“Inadaiwa mlimtomasa sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kumbaka bila ridhaa yake, hali iliyomsababishia maumivu makali msichana huyo,” alidai Nasua.

Mbali na Misokia watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Abdulatif Makila (16), Salum Kiding’a (21), Issa Mfaume (18), Antony Kyulure (16), Kazumari Iddy (15), Kareem Kibwana (15).

Wengine ni Robirn Robert (18), Boniface George (18) na Alen Lwamba (18).

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 21 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali na watuhumiwa wapo nje kwa dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles