33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KIKONGWE AUAWA AKITUHUMIWA KWA UCHAWI

download

Na  Walrer   Mguluchuma-Sumbawanga

MWANAMKE aitwaye   Noelia    Pintilila   (80)   Mkazi wa   Kijiji  cha    Kanyezi   Tarafa ya   Mwazye,   Wilaya  ya  Kalambo  mkoani Rukwa  ameuwawa  kwa kupigwa kichwani na   fimbo baada ya kutuhumiwa  kuwa  ni  mchawi .

Kamanda wa  Polisi wa  Mkoa wa  Rukwa,   Geoge   Kyando   aliwaambia  waandishi wa  habari  jana  kuwa  tukio  hilo lilitokea  juzi  saa  tano   asubuhi  kijijini  hapo .

Alisema  siku  hiyo ya  tukio  marehemu  alikuwa  nyumbani  kwake  akiwa  anaendelea  na  shughuli ndogo  ndogo  za  kila  siku  mara  baada ya  kuwa   amemaliza  kunywa   chai  ya  asubuhi .

Kamanda  Kyando   alieleza  wakati marehemu  akiwa   anaendelea  na  shughuli  zake    alifika   mtuhumiwa wa  mauaji  hayo   ambae  jina   lake   limehifadhiwa    alikuwa ni mgonjwa wa kifafa  na  ndipo   alipomshuku  marehemu  kuwa   ni   mchawi  amemroga  ugonjwa wa kifafa .

Hata  hivyo marehemu    alimkatalia  kuwa  yeye  si  mchawi  na  wala  tabia  hiyo ya  ushirikina   tangu   kuzaliwa   hajawahi  kuwa nayo.

Licha ya kujitetea  huko  mtuhumiwa huyo  aliendelea   kumshutumu   kikongwe huyo kuwa  yeye   ni  mchawi  na  ndiye   aliyemroga   ugonjwa wa kifafa.

Baada  ya  mabishano  hayo  kuendelea   kwa  muda  mrefu   ndipo  mtuhumiwa  alipoanza  kumpiga kwa  fimbo   kichwani  marehemu  Noelia   hadi kufariki   dunia   hapo  hapo .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles