28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 22, 2023

Contact us: [email protected]

MIMBA ZA UTOTONI ZAONGEZEKA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu.

MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM.

UTAFITI mpya wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria kwa mwaka 2015 na 2016 umemulika matatizo makubwa yanayoitesa Tanzania.

Utafiti huo uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ulizinduliwa jijini Dar es Salaam jana, ambapo moja ya tatizo lililoonekana kuongezeka ni mimba za utotoni.

Kwa mujibu wa utafiti huo, tatizo hilo limeongezeka kutoka asilimia 23 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 27 mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu alisema watoto wa kati ya miaka 15 na 19 wameendelea kupata ujauzito na kuharibiwa malengo yao.

“Kiwango cha maambukizi ya malaria kwa watoto bado uko  juu na kuongezeka kutoka asilimia 9 mwaka 2010 hadi asilimia 14 mwaka 2015-16,”alisema Mwalimu.

Mwalimu alisema kuwa ripoti ya utafiti huo umewaumbua wanawake wa mjini baada ya kuonyesha kuwa wanawake wengi wanatatizo la unene na uzito wa kupitiliza, kati ya wanawake 100 ni 42 ambao wanatatizo hilo.

“Wanawake wa vijijini ni 21 kati ya 100 wenye tatizo hilo, tunaanzisha mpango wa mazoezi ili badala ya kutibu watu hospitalini wanaotokana na magonjwa ya uzito tuwe tumeyakinga kwa kufanya mazoezi,” alisema Mwalimu.

Aidha alisema kuwa utafiti huo ulionyesha kuwa kunatatizo kubwa la matumizi ya vyoo bora katika  maeneo ya vijijini kwani kati ya kaya 100 ni kaya 19 zenye vyoo bora.

“Siwezi kuwa mtu wa kutoa matamko kila siku kuhusu kipindupindu wakati watu wengine hawataki kujikinga, haiwezekani kaya nyingine mathalani Njombe ziweze kuwa na vyoo bora kwa asilimia 98 halafu halmashauri zingine zishindwe kusimamia hilo katika mikoa yao,”alisema Mwalimu.

Alisema pia utafiti huo unaonyesha kuwa hakuna mabadiliko makubwa ya vifo vitokanavyo na uzazi, mwaka 2004  hadi 2005 walifariki 578 kwa vizazi 100,000 tofauti na mwaka 2015  na 2016 walifafiki 556 kwa vizazi 100,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,089FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles