26.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Upelelezi kesi watumishi wa BoT bado

Na Imani Nathaniel, Dar es Salaam

Upelelezi wa kesi inayowakabili watumishi wananane wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na wenzao watano bado haujakamilika. 

Watumishi hao wakikabiliwa na mashitaka sita likuwemo kuharibu noti 460,000 za 10, 000 na kuisabaishia benki hiyo hasara ya Sh bilioni 4.6 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam .

Watumishi hao wa BOT ni Mariagoretha Kuzugala, Henry Mbowe, Asha Sekiboko, Cecilia Mpande, Agripina Komba, Zubeda Mjewa, Khadija Kassunsumo na Mwanakheir Omary. 

Washitakiwa wengine ni Alistides Genand, Shukuru Mchegage, Musa Chengula, Zaituni Chihipo na Respicius Ishengoma.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashidi Chaungu, wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai, kesi hiyo imekuja kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamlika. 

Kutokana na hilo, akaiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili kutaja shauri hilo hivyi itatajwa tena Januari 11 mwaka 2021.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kwamba kati ya Januari mwaka 2017 hadi Septemba 30 mwaka 2019, watumishi hao wa BOT kwa kuvunja majukumu yao ya kazi waliwezesha utendekaji wa kosa la kuongoza genge la uhalifu. 

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa, katika tarehe hizo na maeneo hayo, jijini Dar es Salaam, washitakiwa  Genand, Mchegage, Chengula,  Chihipo na Ishengoma wakiwa si watumishi wa BoT, kwa kushirikiana na watumishi hao wa BoT kwa makisudi, waliwezesha kutendeka kosa la uharifu wa kupanga. 

Katika shitaka la tatu , ilidaiwa kwamba, katika tarehe hizo jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote bila ya kuwa na kibali na kutokuwa wazalendo, waliharibu noti kwa kukata noti 460,000 za 10,000 sawa na Sh bilioni 4.6.

Ilidaiwa kuwa, katika tarehe na maeneo hayo, jijini Dar es Salaam, kwa mawasilisho ya kilaghai, kwa kujua na kwa mpango wa kitapeli washitakiwa wote walijipatia faida ya sh bilioni 1.533 kutoka BoT baada ya kuwasilisha noti hizo. 

Shitaka la tano la utakatishaji fedha ilidaiwa kuwa watumishi hao wa BoT  na wenzao hao walijihusisha katika miamala tofauti ya Sh bilioni 1.533 wakati wakijua zilitokana na kosa tangulizi la uhalifu wa kupangwa na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. 

Katika shitaka la sita, washitakiwa wote katika tarehe hizo jijini Dar es Salaam, waliisababishia BoT hasara ya Sh bilioni 4.6.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles