27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Uongozi Tembo Nickel wakaa mguu sawa kuchimba madini

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Uongozi wa Kampuni ya Tembo Nickel Corporation (Tembo Nickel) imekutana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge kujitambulisha rasmi kwa ajili ya kuanza uchimbaji wa Madini hayo.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja mkazi hapa nchini wa Tembo Nickel, Benedict Busunzu katika Mkutano uliofanyika mjini Bukoba katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Busunzu amesema kuwa lengo la mkutano huu nikujitamburisha pamoja na kupata baraka kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera ili kuanza rasmi kwa shunghuli za mradi.

Hata hivyo, amesema kuwa baada ya kukabidhiwa Leseni Maalum ya uchimbaji wa Madini tunaanza rasmi kuwashirikisha wanajamii wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka eneo la mradi ili kuanza kazi Rasmi.

“Tunategemea mwaka ujao shunghuli Kuu zitahusisha marejeo ya upembuzi yakinifu wa uchimbaji Madini kabla ya kuanza shunghuli nzima za ujenzi ambapo, shughuli tunazozitegemea kuanza mara moja zitahusisha mpango mdogo wa uchorongaji na kukamilisha utafiti kwaajiri ya mtambo wa uchenjuaji, ikiwa nipamoja na kushirikisha jamii katika mpango wa makazi mapya kupisha eneo la mradi.

“Katika kipindi cha ujenzi takribani ajira 1,000 kupitia wakandarasi wetu zitahitajika na kipaumbele cha ajira na mafunzo itakuwa kwa Wakazi wa Mkoa huu,” amesema Meneja Busunzu

Aidha, serikali itanufaika na kodi na katika uzarishaji wa Madini itapata asilimia 16 na Tembo Nickel itapata asilimia 84 katika mapato yatakayopatikana Serikali itapata asilimia 50 na Kampuni ya Tembo Nickel itapata asalimia 50.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa wananchi wa Wilaya ya Ngara watapata mapato .

“Wananchi wa Ngara watapata Frusa ya kufanya shunghuli Mbalimbali za kujiongezea kipato na Serikali inategemea kupata mapato mengi kupitia ushuru wa huduma,” amesema Mbuge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles