27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi wa Marekani aridhishwa na huduma za Afya Bugando

Na Sheila Katikula, Mwanza

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald Wright ameeleza kuridhishwa na miundombinu na huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Bugando.

Wridght ameeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza baada ya kufungua maabara ya kisasa ya kufanyia vipimo vya magonjwa mbalimbali katika hospitali hiyo.

Wright amesema amefurahishwa na utendaji kazi wa hospitali hiyo sambamba na ukarabati wa maabara ya kisasa iliyofadhiliwa na ubarozi wa marekani ili kutoa huduma ya vipimo tofauti.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda Bugando, Dk. Fabian Masaga amesema maabara hiyo itafanya vipimo vya viral load Hiv, Hepatitis B,S aratani na vipimo vya Covid-19.

Masaga amesema ubalozi wa Marekani umetoa msaada mkubwa katika kuhakikisha maabara inakamilika kwani tangu mwaka 2005 ndiyo ushirikiano ulianza kati yao.

Mkurugenzi wa Shirika la Management and Development for Health (MDH), David Sando amesema kupitia ufadhili wa watu wa Marekani wamekuwa wakisaidia huduma za maabara kwa ubora unaotakiwa.

Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa ushirikiano ni kitu kizuri katika maendeleo ni vema kudumisha ushirikiano huo ili muweze kufikia malengo  kwa kutoka huduma bora za afya katika Jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles