27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

DCEA kuja na muongozo wa kutoa elimu namna ya kujiepusha na dawa za kulevya

Na Mohammed Ulongo, Morogoro

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imesema kuwa tayari imeandaa muongozo kwaajili ya kutoa elimu kwa jamii kwa lengo la kuielimisha namna ya kujiepusha na matumizi ya Dawa za kulevya.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Novemba 10 na Kamishna Msaidizi Kinga na Huduma za Jamii wa Mamlaka hiyo Moza Makumbuli alipokuwa akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha waandishi wa habari za Kidigitali kinachofanyika mkoani Morogoro.

Amesema kuwa Muongozo huo unalenga kuyafikia makundi mbalimbali yakiwemo watoto waliopo kwenye shule za Msingi na Sekondari, pamoja na vyuo vya ngazi mbalimbali.

Pia Mpango huo unalenga kuyafikia makundi ya watu walio nje ya mifumo ya elimu, watumiaji wa Dawa za kulevya, Wazai/Walezi , viongozi wa kijamii, na Waandishi wa habari.

“Lengo la Mpango huu ni kuyafikia makundi yote kwenye jamii na kuwaelimisha ili wao wakielimika waweze kufikisha elimu hiyo kwenye Jamii zao kwa usahihi.

“Hadi sasa tayari muongozo huo umefikia asilimia 90 naunatarajiwa kuanza kutumika rasmi mwishoni mwa mwaka huu wa fedha.

“Ninaamini kufikia mwisho wa mwaka huu wa fedha mpango huu utaanza kutumika rasmi na tunaimani utawasaidia jamii kupata elimu sahii na mbinu za kupamabana na tatizo hili,” amesema Moza.

Awali, akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi hicho Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka (DCEA), Florence Khambi amewaeleza waandishi wa habari juu ya umuhimu wao katika kuhakikisha wananchi na jamii yote kwa ujumla inapata elimu na ufahamu wa kutosha ya namna inavyoweza kushirikiana na Mamlaka hiyo kuweza kutoa taarifa mbalimbali za uharifu wa Dawa za kulevya kwenye maeneo yao.

“Kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Gerald Kusaya niwahakikishie kuwa, mtu au watu ambao wataleta taarifa zao katika mamlaka zinazohusiana na uhalifu wa Dawa za kulevya, tutazipokea kwa uaminifu wa hali ya juu na tutamtunzia siri, hivyo msiwe na hofu yoyote kama mna taarifa,”amesema Kambi.

Kikao Kazi hicho cha siku tatu kilichoandaliwa na Mamlaka hiyo kimewakutanisha waandishi wa habari za Kidigitari kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Mamlaka hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles