‘UNAWEZA’ YA JAY DEE KUPAMBA MKESHA WA PASAKA

0
1042

NA JESSCA NANGAWE   |   

MKONGWE wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’, anatarajia kufanya tamasha la aina yake siku ya mkesha wa Pasaka katika Ukumbi wa Golden Tulip kwa ajili ya kuutangaza wimbo wake wa ‘Unaweza’.

Akizungumza jana alipotembelea ofisi ya New Habari, inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba na Rai iliyopo Sinza Kijiweni, Lady Jay Dee, alisema tamasha hilo litasindikizwa na wasanii mbalimbali kama Bushoke, Nick Mbish, Alawi Junior na wengine wengi.

“Wimbo wangu wa ‘Unaweza’ utaanza kusikika kesho ‘leo’ katika vituo mbalimbali vya habari na siku ya mkesha wa Pasaka tutafanya tamasha katika ukumbi wa Golden Tulip kwa kiingilio cha Sh 10,000, nategemea sapoti kubwa kwa mashabiki wangu kwani nimejipanga kuwafurahisha,” alisema Jay Dee.

Aliongeza kwa kusema wimbo huo mpya amemshirikisha msanii kutoka nchini Jamaica, anajulikana kwa jina la Luciano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here