24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

OMARION: NAONGEA KISWAHILI SAA 24


NEW YORK, MAREKANI   |

MKALI wa muziki nchini Marekani, Omari Grandberry ‘Omarion’, ametumia ukurasa wake wa Twitter kujisifia jinsi anavyoweza kuongea Kiswahili kwa saa 24.

Wiki moja iliyopita msanii huyo alikuwa nchini Kenya kwa ajili ya uzinduzi wa albamu ya msanii kutoka Tanzania, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, ijulikanayo kwa jina la A Boy From Tandale.

Katika albamu hiyo, Omarion ameshirikishwa kwenye wimbo wa African Beauty, hivyo kuna baadhi ya sehemu ameimba kwa maneno ya Kiswahili na ameweka wazi kwamba anajua Kiswahili na anaweza kuongea kwa saa 24.

“Kama haujawahi kunisikia nikiimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili basi tafuta albamu ya A Boy From Tandale ambayo inapatikana kila kona kwenye mitandao ya kijamii na utanisikia nikiimba kwa Kiswahili. Naweza kuongea Kiswahili kwa saa 24,” aliandika Omarion.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles