31.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

KUTANA NA MTOTO ALIYEZALIWA NA MKIA ANAYEABUDIWA KAMA MUNGU


JOSEPH HIZA NA MTANDAO   |  

MVULANA mdogo aliyezaliwa na mkia unaofikia urefu wa inchi saba alikuwa akiabudiwa kama Mungu na watu wa jamii yake.

Arshid Ali Khan aliyekuwa na miaka 13 kabla mkia huo kuondolewa, alikuwa akiathiriwa ukuaji wake kutokana na mkia huo ingawa ulimfanya aonekana kama alama ya uponyaji katika Jimbo la Punjab nchini India.

Mtoto huyo aliyekuwa akitumia cha watu wenye ulemavu amekuwa akiabudiwa na watu wa jamii yake kama Mungu aliyepewa jina la Balaji.

Khan alikuwa akisema mkia huo amepewa na Mungu na anaabudiwa kwa sababu ni Mungu huyo huyo ndiye anayemuomba ambapo maombi ya watu hugeuka kuwa kweli.

Anasema hajisikii vizuri wala vibaya kuwa na mkia huo yeye anaona vyovyote ni sawa tu.

Arshid sasa anaishi na babu yake Iqbal Qureshi, na wajomba zake wawili baada ya baba yake kufariki dunia akiwa na umri wa miaka sita na mama yake kuolewa tena.

Babu yake, Qureshi, ambaye ni mwalimu wa muziki alisema; “Wakati alipozungumza kwa mara ya kwanza, akiwa na umri wa mwaka mmoja, yote aliyozungumza yalikuwa majina ya miungu kutoka dini tofauti.

“Ilikuwa siku hiyo nilipobaini kuwa ana kitu maalumu kiroho.’

Aliongeza; ‘haijalishi iwapo ni Waislamu au Wahindu, nadhani kuna njia moja tu ya kiroho.’

Nyumbani kwa akina Arshid kuligeuka kuwa hekalu, ambako waumini wake humtembelea kupokea baraka na kugusa mkia wake.

“Maombi ya watu wengi yameitikiwa baada ya kumtembelea.

“Wakati mwingine wenzi wasio na watoto huja kwa Balaji kuomba msaada. Huwabariki na mara nyingi wanatunga mimba,” alidai Qureshi.

Hata hivyo, Arshid mara nyingi alikuwa anapata shida kupanga muda wake katika kuhudumia waumini wake, kuhudhuria shule na kucheza na marafiki zake.

Anasema; “Mara nyingi siku za wiki naenda shule, lakini ninapokuwa likizo au siku za Jumapili watu 20 hadi 30 huja kuniona nyumbani.

Aliongeza; “Si kitu rahisi. Kila mtu anataka kuona mkia wangu, kupokea mbaraka na huuliza maswali tena na tena.

Pamoja na kile kinachodaiwa kuwa na nguvu za kiroo, Arshid alikuwa akitumia baiskeli ya magurudunu wakati mwingine kuchechemea au kupata shida kuinama.

Baadhi ya madaktari nchini India waliiambia familia yake kwamba hali hiyo, inatokana na udhaifu wa mifupa lakini wengine walisema imetokana na ukuaji wa mkia kukwaza uti wake wa mgongo.

Madaktari walishauri kuondoa mkia huo ingawa familia yake ilikuwa ikisema ni bora aendelee kuwa nao kuliko operesheni ya kuhatarisha maisha.

Lakini Qureshi alisema ni Balaji anayapaswa kuamua abaki na mkia au uondolewe.

Kwa upande wake Arshid alionekana yu tayari kuondolewa mkia huo, akisema anaamini kwamba haitazuia watu kuendelea kumiminika nyumbani kwake kufuata Baraka.

Hata hivyo, mwaka uliofuata, akiwa na miaka 14 mtoto huyo aliweza kuondolewa mkia huyo na kutembea kama kawaida.

Baada ya operesheni hiyo, hata hivyo Balaji alionekana kubadili kauli kuhusu uungu wake, akisema anataka kuwa mwalimu wa muziki atakapokuwa mkia. Nina furaha sasa kuwa operesheni ilikuwa ya mafanikio.

“Watu wataacha kuniita Mungu. Sikuipenda hali hii kwa sababu niliamini mimi ni mtoto wa kawaida,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles