27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

UNAKUBALI MTOTO WAKO AUMIE KWA SABABU YA UREMBO?

 

 

NA AZIZA MASOUD,

WAZAZI wamekuwa na tabia za kuwasuka watoto wa kike ama kwa hiari au kwa kuwalazimisha, lengo ni  kuwapendezesha kimwonekano.

Hakuna kipindi ambacho watoto wanaumia kama msimu ambao wazazi wanalazimisha mtoto asuke mtindo ambao unakuwa  mgumu, mara nyingi inakuwa mitindo inayosukwa sana na watu wazima.

Pamoja na kupata maumivu, pia unamfanya mtoto atumie muda mrefu kukaa.

Siyo vizuri kuiga kila tunaloona bila kufuatilia na kubaini athari zinazoweza kutokea, kabla ya kutumia kitu ni vizuri kufanya utafiti na uamuzi wa kukitumia au kukiacha kifanywe baada ya kupima faida na hasara zake.

Si mbaya mtoto kupendeza, lakini unapaswa kuangalia aina ya urembo na mapambo unayomweka.

Kusuka kwa watoto si tatizo kama atakuwa amefikisha umri fulani, lakini tatizo la wazazi unakuta anamsuka mtoto wa miaka miwili au mwaka mmoja bila kujali kama utosi ama ngozi ya kichwa haijakomaa.

Unaweza kumsuka mtoto lakini si lazima umsuke nywele ambazo zitamletea maumivu.

Ukienda kwenye saluni za watoto utakuta mzazi kakaa anamsimamia mtoto anasuka huku analia, lakini anamlazimisha mpaka amalize bila kujali kama anaumia.

Si sawa kufanya hivyo, wazazi wanapaswa  kufahamu kuwa kusuka kunaenda sambamba na kuvuta ngozi ya kichwa na kusababisha maumivu endapo utakuwa na ngozi laini.

Si kuumiza ngozi tu, kuna nywele nyingine unasuka hata mtu mzima unasikia mpaka mishipa ya kichwa inauma. Je, kwa watoto unadhani maumivu yake yanakuwaje?

Maumivu yote unayoyahisi mtu mzima unadhani mtoto anaweza kuvumilia hali hiyo, kwani mtoto asiposuka atapungukiwa nini.

Kama mmeshachunguza watoto wanaoanza kusukwa nywele mapema sura zao huwa zinaonekana kukomaa na baadhi yao mwonekano wanaokuwa nao hauendani na umri wao.

Kwa kuzingatia hilo, mzazi unatakiwa kuanza kumsuka mtoto akiwa na angalau miaka mitano.

Miaka mitano mtoto anakuwa ameshakomaa utosi na kama utaweza bora uwe na utaratibu wa kumkata nywele mpaka atakapokuwa mkubwa, muda ambao atakuwa anajiamulia mambo yake mwenyewe.

Siamini kama urembo wa nywele kwa mtoto ni wa kuzingatia, kwakuwa kwanza katika kipindi hicho anakuwa bado hajajua maana ya urembo.

Kuna watoto wengi tunawaona wanakata nywele na wanavalishwa vizuri bado wanapendeza na kuonekana warembo, wazazi wanapaswa kuwa makini katika vitu ambavyo si vya lazima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles