30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS BASHIR AMKATALIA TRUMP

RAIS wa Sudan, Omar el-Bashir

 

 

KHARTOUM, SUDAN

RAIS wa Sudan, Omar el-Bashir, amekataa mwaliko kutoka utawala wa Saudia Arabia wa kuhudhuria mkutano wa mataifa ya Kiislamu ambao Rais Donald Trump atakuwa mgeni rasmi.

Bashir, ambaye alitoa sababu za kibinafsi, anasakwa kwa uhalifu wa kivita katika eneo la Darfur na Marekani ilikuwa haikufurahia mwaliko wake katika mkutano huo.

Sudan ilikuwa imesema kuwa inataka kuimarisha uhusiano wake na Marekani katika mkutano huo.

Saudia ndilo taifa la kwanza la ziara ya kigeni ya Trump. Taarifa ya Ofisi ya Rais Bashir ilisema kuwa rais huyo aliomba msamaha kwa Mfalme Salma wa Saudia kwa kushindwa kuhudhuria mkutano huo wa Riyadh.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa juu ya uamuzi huo. Waziri wa masuala ya mataifa ya kigeni, Taha al-Hussein, atamwakilisha.

Mwaka 2002 na 2010, mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita (ICC) ilitoa agizo la kukamatwa kwa Rais Bashir kwa mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhaifu dhidi ya binadamu katika eneo la Darfur, ambapo takriban watu 300,000 waliuawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles