25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

UN yapiga kura kupunguza wanajeshi Somalia

NEW YORK, UN

UMOJA wa Mataifa umekubaliana kupunguza idadi ya askari 1,000 wa kulinda amani chini ya ujumbe wa Jeshi ka Kulinda Amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa mpito wa muda mrefu ili kuruhusu uumbaji na ukuaji wa nguvu ya usalama wa Somalia.

Askari wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia watapungua kwa kiwango cha juu cha 19,626 ifikapo Februari 28, 2020.

Mpango huo wa mpito ulianzishwa mwaka 2017 na mipango ya kutoa kikamilifu udhibiti kwa majeshi ya Somalia mwaka 2021.

Azimio hilo linasema kuwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika utafanya kazi ili kuamua kama uwepo mkubwa wa polisi utahitajika katika uchaguzi ujao nchini humo.

AMISOM ilianzishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuanzisha shughuli za kulinda amani wakati wa awamu ya hivi karibuni ya vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia. 

Umoja huo wa kijeshi unajumuisha askari kutoka Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya na Uganda ambao hutumiwa kusini na katikati mwa Somalia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles