27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

UN: Njaa itaua mamilioni Afghanistan

KABUL, Afghanistan

UMOJA wa Mataifa umeonya kuwa janga la njaa litaua mamilioni ya wananchi wa Afghanistan, wakiwamo watoto, kama hazikuwapo juhudi za makusudi kuisaidia nchi hiyo ya barani Asia.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa WFP (Mpango wa Chakula Duniani ulio chini ya UN), David Beasley, sasa Afghanistan ina watu milioni 22.8 wanaohaha kupata chakula, ukilinganisha na milioni 14  waliokuwapo miezi miwili iliyopita.

“Watoto watakufa. Watu watateseka kwa njaa. Mambo yatakuwa mabaya sana…” amesema Beasley akizungumzia hali ya Afghanistan, nchi inayoongozwa na wanamgambo wa Taliban waliorejea madarakani miezi miwili iliyopita.

Kwa upande wake, UN kupitia WFP inataka kiasi cha Dola za Marekani milioni 220 kwa mwezi ili kuweza kukabiliana na hitaji la watu milioni 23 wanaoteseka kwa njaa katika Taifa hilo la Kiarabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles