27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ulimwengu afanya mauaji Kongo

ULIMWENGUNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayechezea timu ya TP Mazembe (DRC), Thomas Ulimwengu, juzi amefanya makubwa baada ya kufunga mabao mawili yaliyoisaidia timu yake kuwafunga watani wao, FC Lupopo 4-1.

Timu hizo kila zinapochuana zimekuwa zikionyesha upinzani mkubwa, hasa kutokana na uhasama mkubwa waliokuwa nao kama zilivyo timu za Simba na Yanga kwa Tanzania.

Ulimwengu ‘Rambo’ aliyekuwa kwenye kiwango bora, alifanya mauaji hayo katika mashindano maalumu ya urafiki yaliyomalizika juzi, mabao mengine ya Mazembe yalifungwa na Cheibane Traore na Adama Traore, huku Clovis Mbayi akiifungia Lupopo bao la kufutia machozi.

TP Mazembe, iliyoukosa ubingwa wa Ligi Kuu Kongo msimu huu uliochukuliwa na AS Vita, imemaliza vema michuano hiyo kwa mafanikio na kufuta machungu ya kushika nafasi ya pili kwenye ligi.

Ulimwengu na Mtanzania mwingine, Mbwana Samatta, wanaokipiga kwa matajiri hao wa jiji la Lubumbashi, wameitwa na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Mart Nooij, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa  kufuzu Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017 dhidi ya Misri, utakaofanyika Juni 14, jijini Alexandria, Misri.

Mbali na kucheza na Misri, Stars, iliyopangwa Kundi G, itacheza na kigogo kingine cha Afrika, Nigeria pamoja na Chad, ambao wanaonekana kama vibonde.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles