24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Uefa na njama za kujitoa Fifa

NYON, USWISI

BARAZA la Vyama vya Soka Ulaya (UEFA), lipo kwenye njama za kujitoa katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na kuandaa mashindano pinzani, ikiwa ni jitihada za nguvu za kufanya mageuzi kwa kumwangusha Sepp Blatter, imeelezwa.

Njama hizo za Uefa zinatokana na rushwa ya Dola za Kimarekani milioni 100 inayoikabili Fifa, zilizolipwa kwa haki ya matangazo ya televisheni, mikataba ya udhamini na kura wa Kombe la Dunia.

Hongo hiyo inadaiwa ilitumika kufanikisha uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia kwa Russia (2018) na Qatar (2022), huku England na Marekani zilizoonekana vigogo kwenye uombaji zikitoswa, hadi sasa maofisa saba wa Fifa wanashikiliwa na vyombo vya usalama vya Marekani kuhusu rushwa hiyo.

Inaelezwa kuwa Uefa, yenye wanachama 54, imepanga kuandaa mashindano ya Ulaya kila baada ya miaka miwili na kualika mataifa makubwa mengine nje ya bara hilo, hiyo yote wakitaka kupambana na kashfa ya rushwa ya Fifa.

Mpango huo wa kujitoa Fifa ulijadiliwa kwenye mkutano wa Uefa uliofanyika Ijumaa iliyopita kabla ya Uchaguzi wa Fifa uliomsimika tena madarakani Blatter (79) kwa awamu ya tano.

Uefa itafanya kikao cha Kamati Tendaji jijini Berlin baadaye wiki hii na majadiliano yatahusisha nchi zote 54, ambapo watatoka na jambo jingine kuhusu suala hilo kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Barcelona na Juventus Jumamosi hii.

Wakati huo huo, Waziri wa zamani wa Qatar, Sheikh Hamad bin Jassim bin Jaber al-Thani, amekana madai kuwa nchi yake ilitoa rushwa kubwa iliyowafanya kushinda uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2022.

Alisema madai hayo yametengenezwa na nchi ambazo hazitaki ‘ushindani wa haki’. “Angalia jinsi zisivyoiongelea Russia, wamekuwa wakiishutumu Qatar,” aliuambia mtandao wa Fox News juzi.

“Tunaiunga mkono bila shaka Russia, kwa uandaaji wao 2018. Lakini tunaona mazungumzo …yanaizungumzia Qatar, kwa sababu imetokea kwenye nchi ndogo ya Kiarabu, nchi ya Kiislamu. Hivyo ndivyo watu wanavyojisikia.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles