Mashabiki wamaliza ubishi wa Ney na Diamond

0
764

diamond nayNA MWANDISHI WETU

MASHABIKI jijini Arusha walimaliza ubishi uliokuwepo kati ya wasanii wa kizazi kipya, Elibariki Emanuel ‘Ney wa Mitego’ na Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’ waliokuwa wakibishana stejini kupitia wimbo wao wa ‘Mapenzi pesa ama Ujuzi’.

Tukio hilo lilitokea katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jumamosi iliyopita, wakati Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea urais.

Katika shoo yao hiyo iliyochengua mashabiki, Diamond alisimamia upande wa mapenzi pesa, wakati Ney alisimama upande wa mapenzi ujuzi.

Ney yeye akaamua kuuliza mashabiki wangapi wanasema mapenzi pesa na wangapi wanadai mapenzi ujuzi, ndipo umati wa mashabiki wao walipolipuka kwa kelele kwamba mapenzi pesa huku wakibeza kwamba ujuzi upelekwe Chuo cha Ufundi ‘Veta’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here