22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

Casillas atema nyongo Simba

NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KIPA wa timu ya Simba, Hussein Shariff ‘Casillas’, amesema hayupo tayari kutolewa kwa mkopo kwenda timu nyingine, huku akidai bora aache kabisa kuitumikia timu  hiyo na kuwa mchezaji huru.

Cassilas amekuwa majeruhi kwa muda mrefu baada ya kuumia goti walipokuwa kambini nchini Afrika Kusini mwaka jana, hali iliyopelekea kukaa muda mrefu bila kucheza, ambapo inadaiwa uongozi wake unataka kumtoa kwa mkopo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Cassilas alisema yupo tayari kuondoka Simba, lakini si kwa kutolewa kwa mkopo na kusisitiza kuwa anajiamini kutokana na uwezo mkubwa wa kudaka aliokuwa nao.

“Najiamini na kazi yangu ndiyo maana mpaka sasa timu yangu inanihitaji kutokana na kazi yangu ninayoifanya, isitoshe, nimeshakuwa kipa bora kwa misimu miwili mfululizo, kwa hilo najivunia,” alisema.

Alisema atakaporudi kazini ataendelea kufanya vizuri zaidi, hivyo mashabiki wategemee mambo mazuri zaidi atakaporudi dimbani rasmi kutokana na kumkosa kwa muda mrefu alipokuwa majeruhi.

Kamati ya Usajili ya Simba chini ya Mwenyekiti, Zacharia Hans Poppe, wameiongezea nguvu safu ya langoni baada ya kuonekana kulegalega msimu uliopita na kupelekea Simba kushika nafasi ya tatu.

Mpaka sasa imemsajili kipa mpya kutoka JKU ya Zanzibar, Mohamed Abraham Mohamed, aliyefanya safu hiyo kuwa na makipa watano, wengine wakiwa ni mkongwe, Ivo Mapunda, Manyika Peter Jr,  Casillas pamoja na kipa aliyepandishwa kutoka timu ya vijana, Denis Richard.

Hivyo, kuna hofu kubwa ya Casilas na Richard kuenguliwa kwenye usajili wa timu hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles