30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ukiwa na sifa hizi, mwanamke hakuachi – 2

happy-african-american-couple

HAKUNA aliye kwenye uhusiano anayetamani kuacha, kuchwa au kuachana na mpenzi wake ikiwa wana mapenzi ya dhati.

Wachache ambao nia zao za ndani hazina dhati ya mapenzi wanaweza kuwa wa namna hiyo. Lakini ukweli ni kwamba  wanaume wengi kutokana na majukumu ya kukimbizana na maisha, hawafikirii sana kuhusu uhusiano na wenzi wao.

Wanawake wana nafasi kubwa ya kutafuta furaha na namna ya kuwapagawisha wanaume zao tofauti na wanaume. Hali hiyo husababisha wanawake kuwa na wanaume wengine nje au wakati mwingine kuwakacha wanaume zao.

Katika mada hii iliyoanza wiki iliyopita, najaribu kueleza yale mambo ya msingi zaidi ambayo ikiwa mwanaume atakuwa nayo, atakuwa kwenye nafasi kubwa ya kudumu na mwezi wake.

Tayari tulishaanza kuona baadhi ya mambo muhimu wiki iliyopita, sasa leo tuendelee kuona ni mambo gani hayo yanayozingatiwa na wanawake wengi.

UWE MTU WA KUJALI

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.

Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.

UKARIBU

Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.

Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.

Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa!

 

KUMSIFIA NI UCHAWI

 Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao.

Unapokuwa na mwenzi wako katika mtoko, mpe nafasi ya kwanza. Msifie kwa wengine na mtambulishe kwa uwazi, siyo kuonyesha nia ya kufichaficha uhusiano wenu.

Kufichaficha kunamfanya ajione asiye na thamani au pengine umemfanya spea tairi, ukiwa na wako mwingine aliye rohoni mwako.

Sikia nikuambie, kumsifia mwanamke kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza kwa makini, hata kunapokuwa na mgongano katika familia, halafu wakatokea wageni, baada ya utambulisho na mazungumzo ya hapa na pale, wageni wakiondoka kunakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika familia.

Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye.

MALENGO

Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika.

Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilika rafiki zangu. Inawezekana wazee wa zamani walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la kununua ng’ombe na kuwaweka katika zizi kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa malisho mazuri, baada ya miaka miwili wanazaliana, hapo ndipo anamweleza mkewe.

Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote.

Yes! Mkeo ndiye ndugu yako maana umetengeneza naye familia. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja.

Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.

Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu.

Mada hii itaendelea wiki ijayo, USIKOSE!

Jiandae kupata kitabu changu kipya cha SIRI ZA NDOA YENYE FURAHA. Kama unakihitaji weka oda yako kupitia 0712 170745  (What’sApp na sms tu).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles