23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

KAZI KAZI HAINAGA MIPAKA YA KIMUZIKI BARANI AFRIKA?

man-fongo56

SIZUNGUMZII ngoma aliyoshirikishwa na Prof Jay, wala siongelei singo zake nyingine zenye ujumbe tata kama ‘Hainaga Ushemeji’ au ‘Hauna Kila Kitu’ au ile aliyopewa shavu na Shilole ‘Mtoto Mdogo Mdogo’.

Nazungumzia mipagawisho iliyomuibua kwa mashabiki yaani Singeli inayobamba kila kona, lakini ukiicheki ‘back’ hadi ‘front’ yake ni muziki flani hivi wenye vikorombwezo kibao uliokitwa kidizaini ya mchanganyiko ulioibukia kwenye mchiriku kupitia mnanda, kisha ikawa kama kitu kilichokosewa kupigwa kwa midundo yake inayotoka nduki kama kumtoa baru panja.

Ndiyo mikito fasheni ya mujini kwa sasa inayobamba kila kona manake imeibua wasanii kibao ambao kwenye mikong’osio mingine wasingepagawisha, kwani pande hizo zinahitaji kulipuka pamba na swaga za kiaina flani hivi zinazotaka uwe na mikwanja ili kumudu kujiseti kihivyo.

Lakini Singeli ni mambo ya uswazi yaliyosonga hadi matawi ya juu na hainaga swaga kivile wala shobo, manake kama iko kisimpo hata msanii akitinga na ndala stejini iko poa tu kama unavyocheki kwenye video zake jinsi wanavyotokelezea kidizaini yao isiyojali makunyanzi na staili za kivyao zisizojali swaga za shobo na kuuza sura.

Singeli ni kazi kazi kwa kwenda mbele na ishu zinazozungumziwa zinatachi wanaoshabikia, Man Fongo alikomaa kikazi kazi na Prof Jay katika ngoma ya ‘Kazi Kazi’ kisha akasaula zake mwenyewe zinazombambisha lakini ni kama ‘back’ enzi zile za studio za kwanza.

Wasanii wa mchiriku walikuwa wakitinga studio hawatumii vinanda vya studio manake vinawazingua hawapati mikito wanayoitaka, walikuwa na vinanda vidogo vya kuchezea watoto kisha ili wapate mzuka lazima pale ‘front’ yao wakati wanarekodi mwana mmoja awe anapiga staili za kuita kupanda na kushuka kwa mikong’osio ya vibati na vinanda.

Manake mnanda kwa asili ni ‘free style music’ mistari inaweza kuchenji any time kutokana na mzuka, kisha stimu zake ni stori za mashemeji watata kama ile ya Msaga Sumu ya kutegwa na shimela.

Sasa msichokinyaka wengi ni kwamba kwa sasa Singeli ipo kila kona hapa kitaa cha Afrika kwa majina tofauti, kutegemeana na lugha inayotumiwa katika sehemu husika.

Kule Misri vibosile waliipinga hadi wakachemsha na sasa inabamba kwenye kila kona na wasanii wa Singeli wa pande hizo wanapiga hela chafu kwa kutinga kwa Wamisri wenzao mamtoni kupiga shoo.

Kisha undava wake ni wa kimeni ingawa kuna ‘Chura’ wa Snura kisingeli lakini ni mikito ya mameni zaidi kuliko mashori, ambao kwenye Singeli zao ni mikatiko ya kuzungusha kiuno kwa spidi namba tatu ya feni.

Kiduku si kiduku, mnanda si mnanda, mchiriku si mchiriku lakini ni mikito fasta kwa chorus simpo zinazobamba kichwani na dizaini kama naanza kukubali kuwa kama kule ‘back’ ilikuwa inaonekana kama mchiriku na mnanda ni uhuni, vipi kama Singeli yenye vionjo vyake ikichukuliwa kama ishara ya muziki wa Kibongo badala ya kuitosa kama ilivyotoswaga achimenengule!?

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles