22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Ukawa wairarua bajeti ya Serikali

mbatiano maoni ya upinzaniNA ARODIA PETER, Dodoma
KAMBI rasmi ya upinzani bungeni imeirarua bajeti ya Serikali na kuainisha mambo mbalimbali yatakayokwamisha utekelezaji wake.
Mbali na hayo, hotuba ya Ukawa ilitoa mchanganuo unaoonyesha kwamba kutokana na ukuaji wa deni la taifa, kila Mtanzania kwa sasa anadaiwa zaidi ya Sh 800,000.
Akisoma hotuba ya kambi hiyo bungeni jana, Msemaji wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa Wizara ya Fedha, James Mbatia alisema si sahihi Serikali kujigamba kuwa mwaka huu bajeti imeongezeka kutoka Sh trilioni 19.8533 kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 hadi kufikia Sh trilioni 22.495 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kwani thamani ya shilingi ya leo ni pungufu ya thamani ya shilingi ya mwaka jana.
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, aliainisha hoja na sera mbalimbali za Ukawa kuhusu ukusanyaji na utumiaji wa mapato ya Serikali endapo wataingia madarakani Oktoba, mwaka huu.
Alisema hii ina maana kuwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2015/2016 ni ndogo kuliko bajeti ya mwaka 2014/2015, kwamba Serikali imeshindwa kuwaeleza Watanzania ukweli wa ongezeko hilo hasi la bajeti ambalo haliendani na thamani ya shilingi kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Alisema matatizo yanayoathiri mfumo wa bajeti ya Serikali ya sasa ni ukosefu wa nidhamu na uwazi katika masuala ya bajeti ambapo pia katika kipindi hiki taifa linashuhudia uwapo wa ongezeko la malimbikizo ya malipo, ambapo bajeti inayopitishwa na Bunge haifanani na bajeti inayotekelezwa na Serikali.
“Makadirio ya mapato ni makubwa kuliko ukusanyaji wa mapato halisi, ongezeko holela la misamaha ya kodi, bajeti tegemezi, matumizi ya kawaida ni makubwa kuliko mapato ya Serikali, matumizi ya kawaida ni zaidi ya fedha za miradi ya maendeleo, kasi ya ukuaji wa deni la taifa na ongezeko la vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyoainishwa na CAG.
“Mheshimiwa mwenyekiti, katika kurudisha misingi bora ya bajeti ya Serikali, tunaamini kuwa Serikali ijayo chini ya Ukawa itarudisha nidhamu ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato, ambapo maamuzi ya Serikali na viongozi ambayo yanahitaji matumizi ya fedha za Serikali katika mwaka wa bajeti au miaka ijayo yanawekwa wazi na kuchambuliwa,” alisema Mbatia

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles