25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ujerumani yatoa bilioni 26.4 kusaidia wakimbizi Kigoma, Kagera

 

balozi-hassan-simba
Balozi Hassan Simba

Serikali ya Ujerumani  kupitia ubalozi wake hapa nchini imetoa msaada wa shilingi bilioni 26.4 kusaidia wakimbizi walioko katika mikoa ya kanda ya ziwa kama vile Kigoma na Kagera.

Kwa mujibu wa Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Kochanke, fedha hiyo itatengwa mara mbili ambapo kiasi kutapelekwa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) na nyingine Shirika la Chakula Duniani (WHO).

“Fedha hizi tumezitenga kwenye mafungu haya kwa sababu kila shirika moja lina majukumu yake kwa wakimbizi, Mfano; WHO lenyewe ni kwa ajili ya kuhudumia chakula na UNHCR linashughulikia mambo mengine kama Afya na usalama,” alisema Kochanke.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba, alisema Tanzania kwa kushirikiana na nchi mbalimbali zinaendelea kushirikiana ili kuhakikihisha wakimbizi wanapungua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles