32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

UJENZI WA KIVUKO KIKUBWA KIPYA CHA BUSISI WAANZA

Na JUDITH NYANGE

-MWANZA

WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), imeanza ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo Busisi  kitakachokuwa na uwezo wa  kubeba tani 250, magari 36 na abiria 1,000 kwa lengo la kuboresha huduma ya usafiri.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kivuko hicho juzi, Mtendaji Mkuu wa Temesa, Dk. Mussa Mgwatu, alisema kivuko hicho kitajengwa na Kampuni ya kizalendo ya  Songoro Marine Transaport Boat Yard Ltd ambayo imeshinda zabuni ya ujenzi unaotarajiwa kukamilika Januari, mwakani.

Alisema ujenzi wa kivuko hicho utafanyika kwa muda wa miezi 12 kulingana na mkataba na tayari vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati (Marine Plate) yamewasili katika karakana ya kampuni hiyo iliyopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuanza ujenzi.

“Lengo la kuongeza kivuko ni kuboresha huduma za usafiri na kuwapunguzia abiria muda wa kusubiri kuvuka, mradi huu unatekelezwa  kupitia bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18 na unatarajia kugharimu Sh bilioni 8.9,  tunategemea mkandarasi atafanya kazi hii kwa haraka kwa sababu wananchi wanasubiri kivuko hiki,” alisema Dk. Mgwatu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transaport Boat Yard Ltd, Salehe Songoro, aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuiamini kampuni hiyo na kuahidi kuifanya kazi hiyo kwa haraka.

“Naishukuru Serikali kwa kuendelea kutuamini sisi wakandarasi wazalendo, kwa sasa kampuni  tumeshajiimarisha kielimu, kivifaa na kiteknolojia  na tupo tayari kufanya haraka zaidi, nia ni kukamilisha kazi hii kwa wakati na kwa ubora zaidi,” alisema Songoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles