Na Mwandishi wetu
UHUSIANO ni mgumu. Ndoa ina changamoto pia lakini inapaswa kila mara kuishi kwa kuchukuliana kwa kila mmoja kumjua vyema mwezi wake na kuweza kufanyia kazi mapungufu yanayojitokeza.
Kwa namna ya pekee linapotokea tatizo unapaswa kulitafakari mara mbili kabla ya kulifanyia kazi ili kuepuka kumkwaza mmoja kati yenu. Kwa namna ya pekee ili uhusiano au ndoa idumu mnapaswa kuishi katika misingi yake pamoja na kufanya haya;
- Samehe
Hata maandiko matakatifu yanaandika kuwa samehe saba mara sabini, hivyo unapokosewa na tayari mko wawili katika uhusiano jifunze kuchukulia na kusamehe. Hata kama kosa ni kubwa jitahidi kutafuta suruhu ili usamehe.
- Sahau
Kama ukisamehe lakini usisahau, hapo umesamehe kweli?
Jifunze kusahau, ninapingana na wenzi ambao wanapenda kuhukumu. Wapo wanaosamehe na linapotokea kosa dogo hujikuta wakikumbushia kutokana na kuweka kitu moyoni.
- Kuweni timu nzuri
Maisha yanakuja unavyoyafanya. Moja ya vitu vizuri kuhusu uhusiano na ndoa ni kuwa na mtu wa karibu ambaye mnabadilishana mawazo. Jifunze kutoka kwa wengine, mtu uliye katika uhusiano naye ambaye atakubadilisha au atajifunza kutoka kwako. usishindane. Jifunze kushukuru.
- Tafuta ukweli
Kuna msukumo mkubwa wa kuamini mtu kutokana na yale ambayo tunayasikia kutoka kwa wengine. Toa mtazamo huo kwa kutafuta ukweli mara kwa mara.
- Safirini pamoja
Kusafiri pamoja kama wenzi kuna nguvu ya ziada ambayo inasababishwa kuimarisha mapenzi kutokana na kuwa karibu zaidi. Hata kama ikitokea mmesafiri tofauti sawa lakini pigeni picha na kutumiana.
- Kuwa na maadili
Usiwe mtu usiyekuwa na staa mbele za watu jaribu kujifunza kuwa mstaarabu na fanya kila uwezavyo ili kumlinda mpenzi wako usimkwaze.
- Kuwa mtu wa majukumu
Kila mtu ana majukumu ya kila siku ambayo anapaswa kuyatekeleza kwa ufasaha, ukiwa baba/mama wa familia unapaswa kukumbuka jukumu lako. Kumbuka pia fedha inahitajika hivyo jifunze kuwa na matumizi mazuri ya pesa.
- Wote mko sawa
Haijalishi nani kati yenu anapata fedha nyingi na kuisaidia familia. Haijalishi nani kati yenu ana kampuni kumbwa inayoweza kuingiza mabilioni. Haijalishi nani ana jina kubwa na anajulikana zaidi. Wote ni sawa.
- Heshimuni marafiki wa kila mmoja
Marafiki ni muhimu pia katika maisha yenu, unajua marafiki zenu mmewapata vipi na mmekutanaje, hivyo kila mmoja anapaswa kuheshimu marafiki wa wengine.
- Jua namna ya kufunga mdomo
Hakuna kitu kizuri kama kuwa na siri na kuweza kuificha kwa kutosemasema vitu vinavyowahusu kwa watu. Hata kama ni marafiki jaribu kuwa na siri na kuweza kufanya
- Rekebisha muonekano wako
Cheti cha ndoa yako hakikupi nafasi ya kuvaa kila mara kawaida pasipo mara moja moja kuwa mtanashati. Jaribu kurekebisha suala la mavazi yako ambayo ndiyo muonekano wako wa kila siku.