28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yasema inawafahamu watoa rushwa majimboni

Faraja Masinde -Dar es salaam

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimeonya na kusema kuwa kinawafahamu kwa majina wanachama wake wote wanaotoa rushwa ikiwamo majimboni na kuonya kuwa kitawakata na kuwakatakata.

Onyo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole alipokuwa akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa mubashara na wananchi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook.

Swali hilo liliulizwa na mfuatiliaji wa matangazo hayo, Hezbin Mtoro ambaye aliyetaka kujua namna kilivyojipanga kudhibiti rushwa katika kipindi cha uchaguzi.

“Katika kipindi cha uchaguzi mara nyingi huwa tunafahamu au imezoeleka kwamba viongozi wengi wa kata huwa wako wazi sana katika sual ala rushwa husususan katika kura za maoni, sasa kama chama mmejipangaje kwa ajili ya kuhakikisha kuwa taifa linapata viongozi sahihi?,” alihoji Mtoro. 

Akijibu swali hilo, Polepole alisema kuwa chama hicho kinawafahamu watoa rushwa wote wa majimbo yote kwa majina na fedha nazotoa na kwamba kitawakata na kuwakatakata.

“Rushwa ni adui wa haki, rushwa haikubaliki na haina nafasi CCM, nipende kuwaeleza kwa msisistizo kwamba tunafuatilia kwa karibu sana sarakasi,vurumai, figisu, ngombelengombele ambazo watu wanaotafuta uongozi kwa hila wanaendelea nazo katika maeneo kadhaa nchini.

“Niseme kwamba tunawafahamu wote mnaotoa fedha, mnahonga wajumbe wa vikao tunawafahamu, kwa majina, kwa vikao mlivyofanya, kwa pesa mlizotoa tunawafahamu, niko leo Dar es Salaam tunawafahamu watoa rushwa wote, wamajimbo yote tunawafahamu.

“Nikueleze ya kwamba uongozi wa awamu ya tano umejipanga kuzuia rushwa, rushwa ni adui wa haki ukitenda rushwa unamudhi hata Mungu, tutawakata na kuwakatakata, tuko nyuma tungaangalia, subiri uje uonea hii sinema itakavyokuwa, ndivyo tuwafundishe adabu wala rushwa kwamba hawana nafasi kwenye hiki chama, na ninyi watu wanyoofu watenda haki kwelikweli endeleeni kuwa waaminifu kwa CCM,” alisema Polepole.

Kuhusu chama hicho kutoa kipaumbele kwa wagombea wanaoishi kwenye maeneo husika, Polepole alisema kuwa kila mtu anahaki ya kuchagua na kuchaguliwa huku akisema kuwa wanaoshi kwenye maeneo husika ndiyo wanaozijua changamoto za wananchi zaidi.

Akijibu swali liloulizwa kama iwapo bado wapinznai ni kama virusi hatarai vya corona Polepole alisema kuwa hakumaanisha hivyo.

“Hii kauli wanaichanganya lakini watu… kitu mnachokifanya siyo kizuri. Nilisema corona haina tofauti na upinzani unaotupinga katika jitihada zetu za kuleta maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles