24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

KIM JONG UN Atokee, asitokee hadharani kila siku gumzo

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI

YUPO kiongozi mmoja kule Korea Kaskazini wengi wanamwona mtaa ajabu anaitwa Kim Jong-Un. 

Yaani kila mara hubeba vichwa vya habari katika magazeti na majarida makubwa duniani.

Utasikia; “Tunatest mitambo”, mara karusha kombora la masafa mafupi, mara lingine kaelekezea baharini karibu na Japan, utasikia tena karusha la masafa marefu. 

Huchelewi kusikia kafuta maofisa wa jeshi, au katimua fulani, au katia mgomo fulani.

Kim Jong- un ni mtoto wa tano na wa mwisho ktk uzao wa Kim jog-il( raisi wa pili wa Korea Kaskazini) na kwa sasa ndo kiongozi wa nchi hiyo na alichukua cheo hicho baada ya kifo cha baba yake Dec 19, 2011.

Kim jong-un anatajwa kuwa mmoja wa viongozi wenye msimamo mkali hasa kwa nchi za kimagharibi na hadi sasa anaimarisha nguvu za kinyuklia za Korea kaskazini.

Huyu jamaa anamnyima usingizi Rais Donald Trump, wa Marekani, China na jirani yake  Korea Kusini.

Aonekane hadharani, asionekane dunia nzima ni habari kubwa, sasa, hivi karibuni alitoweka na hakuonekana kwa siku 20 na akazua gumzo vilevile.

 Lakini baada ya minong’ono mingi kuhusu afya yake, wengine wakienda mbali na kusema amekufa, hatimaye chombo cha habari cha serikali  wiki iliyopita kilitoa picha ya yake , Kim Jong Un ikimwonyesha anafungua kiwanda cha mbolea.

Chombo hicho cha Serikali kilisema Kim Jong ameonekana kwa mara ya kwanza hadharani  baada ya siku 20.

Tetesi kuhusu afya ya Kim zilianza kuenea baada ya kutoonekana katika shehere za maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa babu yake, mwasisi wa taifa hilo Kim Il Sung  Aprili 15  mwaka huu.

Maadhimisho hayo ni moja katika shehere kubwa katika kalenda ya Korea Kaskazini, na kwa kawaida Kim amekuwa akiadhimisha kwa kutembelea eneo ambalo babu yake huyo amezikwa. Kim hajawahi kukosa shughuli hiyo.

Madai juu ya afya mbaya ya Kim kisha yalipatikana katika ripoti ya tovuti inayoendeshwa na wakosoaji wa  Korea Kaskazini.

Chanzo ambacho kilifichwa kililidokeza Daily NK kwamba wanafahamu Kim alikuwa akipambana na tatizo la moyo tangu Agosti mwaka jana “lakini hali ilizidi kuwa mbaya baada ya kutembelea mara kwa mara huko katika mlima  Paektu.

Taarifa hizo kutoka katika chanzo kimoja ndizo zilizosambaa katika vyombo vya habari vya kimataifa.

Mashirika ya habari yalianza kuripoti madai hayo, hadi pale zilipoibuka taarifa kuwa mashirika ya kijasusi ya Korea Kusini na Marekani zinafuatilia madai hayo.

Baada ya hapo vikaibuka vichwa vya habari cha kushtua kwenye vyombo vya habari vya Marekani  kwamba kiongozi huy wa Korea Kaskazini alikuwa katika hali mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo naye alionekana kuongeza mafuta kwenye moto kuhusu tetesi hizo Aprili 29, kwa kusema maofisa wa Marekani hawajamuona Kim hivi karibuni.

Ingawa taarifa kutoka katika Serikali ya Korea Kusini, na vyanzo kutoka ndani ya vyombo vya usalama vya China  vilivyozungumza na Shirika la habari la Reuters – vilisema taarifa hizo si sahihi.

Lakini hii si mara ya kwanza kwa Kim kupotea hadharani, Septemba 2014 hakuonekana kwa siku 40 baada ya kuhudhuria tamasha na alikuja kuonekana katikati ya mwezi Oktoba akitumia fimbo.

Chombo cha Serikali hakikufafanua alikuwa wapi.

Lakini Shirika la Kijasusi la Korea Kusini lilisema huenda wakati huo alifanyiwa upasuaji  mguuni katika eneo la ‘ankle’ kutokana na tatizo maumivu.

Tahadhari mara nyingi hutupwa kando wakati vyombo vingi vya habari vya kimataifa vinaporipoti juu ya Korea Kaskazini. 

Uchekeshaji mwingi, uvumi wa kudanganya unaweza kulisha tasnia inayojua kuwa vichwa vya vya habari vya kichochezi dhidi ya Kim Jong-un ni habari kubwa.

Shirika la habari la KCNA lililoripoti habari hiyo na kishwa kubebwa na vyombo vikubwa vyote duniani lilisema kwamba Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini katika ufunguzi huo wa kiwanda cha mbolea alikata utepe na kushangiliwa sana hali iliyoashiria kuwa uvumi huo si tu kwamba ulikuwa nje ya mipaka ya Korea Kaskazini.

Shirika hilo la habari liliongeza kuwa watu waliokuwapo katika kiwanda hicho walilipuka kwa shangwe baada ya Kim Jong Un kuonekana kiwandani hapo.

Taarifa za kuonekana kwake hadharani zilikuja baada ya mara ya mwisho  kuonekana katika shughuli za kiserikali Aprili 12 mwaka huu huku ikizuka minong’ono kuhusu afya yake.

Shirika la habari la Uingereza la BBC lilisema taarifa hizo mpya kutoka katika chombo cha habari cha Korea Kaskazini haziwezi kuwa za mwisho au huru kuthibitisha kuonekana kwa kiongozi huyo.

Chombo hicho cha habari cha Serikali baadae kilitoa picha kadhaa zikimuonyesha Kim akikata utepe nje ya kiwanda hicho.

Alipoulizwa kuhusu kuripotiwa kuonekana kwa Kim hadharani, Rais wa Marekani Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa hakutaka kuzungumza chochote.

KILICHOSEMWA NA CHOMBO CHA HABARI CHA SERIKALI 

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha serikali cha nchini Korea Kaskazini, Korean Central News Agency (KCNA), katika ufunguzi huo wa kiwanda cha mbolea, Kim alikuwa ameongozana na maofisa kadhaa waandamizi  wa Korea Kaskazini, akiwamo dada yake Kim Yo Jong.

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini alikata utepe kuashirika uzinduzi wa kiwanda hicho katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo katika eneo la Kaskazini Pyongyang.

“Watu waliohudhuria hafla hiyo walilipuka kwa shangwe; ‘hurrah!’  kwa kiongozi huyo wa juu ambaye anaongoza watu wote na kusimamia ustawi wa taifa “, lilieleza KCNA katika taarifa yake.

Kim alieleza kufurahishwa na mfumo wa uzalishaji wa kiwanda hicho, na kukipongeza kwa kuchangia maendeleo ya nchi hiyo husuani katika viwanda vya kemikali na uzalishaji wa chakula, liliongeza shirika hilo la habari.

HUYO NDIO KIM JONG UN Hakuna anayejua kwa uhakika mwaka aliozaliwa zaidi ya kuwako kwa kumbukumbu kwamba alizaliwa  Januari 8, kati ya  mwaka 1982-1984  Julai 5,1984)

Mbali na kuwa Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea (WPK).

Kim ni mtoto wa pili wa Kim Jong-il aliyezaliwa mwaka 1941 na kufariki mwaka 2011 na Ko Yong-hui. Kabla ya kuchukua madaraka, Kim alikuwa haonekani mara kwa mara kwa umma. 

Maelezo kama vile mwaka gani alizaliwa, na kama alienda kweli shule nchini Uswisi akitumia jina la uongo, ni vigumu kuthibitisha.

Tangu mwaka 2009 taarifa zilianza kutokea kuwa Kim aliteuliwa kumfuata baba yake aliyekuwa mgonjwa, akipewa nafasi katika kamati ya kijeshi. Nyimbo zilianza kutungwa za kusifu familia ya Kim zikitaja jina la Kim Jong-Un. 

Mwaka 2010 alipewa cheo cha jenerali jeshini na kuwa makamu wa mwenyekiti wa kamati kuu ya kusimamia jeshi.

Kim alitangazwa kuwa kiongozi mkuu baada ya mazishi ya baba yake Desemba 28 2011. 

Vyeo vyake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea, Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, Mwenyekiti wa Tume ya Mambo ya Ndani, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Watu wa Korea, na mwanachama wa Kamati ya Kudumu ya Politburo ya Chama cha Wafanyakazi wa Korea. Machi 9, 2014, Kim Jong-Un alichaguliwa bila kupingwa kuingia katika Bunge Kuu la Watu wa Korea Kaskazini. Kim ana shahada mbili, moja ya fizikia kutoka Chuo Kikuu cha Kim Il-sung, na nyigine kama ofisa wa Jeshi katika Chuo Kikuu cha Jeshi cha Kim Il-sung.

Desemba12,  2013, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vilitangaza kwamba kwa sababu ya “udanganyifu,” aliamuru mauaji ya mjomba wake Jang Song-thaek. 

Kim Jong-Un anaaminika kuwa ndiye aliyeamuru mauaji ya kaka yake wa kambo, Kim Jong-nam nchini Malaysia mwezi Februari 2017.Inasemekana Nam alikuwa mtu anayempinga sana.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles