27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

‘Uhuru wa habari unapita wakati mgumu’

Roderick LutembekaNa Jonas Mushi, Dar es Salaam

WAKATI dunia ikiadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani jana, Bazara la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limesema uhuru wa habari na upatikanaji wa taarifa nchini unapitia wakati mgumu kuliko kipindi cha ukoloni.

Siku ya Uhuru wa Habari Duniani huadhimishwa Mei 3 kila mwaka kwa madhumuni ya kujikumbusha misingi muhimu   na kutathmini mwenendo wa uhuru wa habari, kuutetea na kuulinda dhidi ya vitisho na mashambulio   na kuwakumbuka waandishi wa habari waliokufa  wakati wakitimiza majukumu yao.

Akizungumza   Dar es Salaam jana kwa niaba ya wazee, Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee   wa Chadema, Roderick Lutembeka, alisema  hujuma, vitisho, vipigo, mauaji na mashambulio dhidi ya haki ya kupata taarifa ni miongoni mwa viashiria vya kutoweka kwa uhuru wa habari nchini.

“Watanzania wanaadhimisha siku hii wakiwa katika sintofahamu kwa sababu uhuru wa habari na upatikanaji wa taarifa kwa ujumla unapitia wakati mgumu kuliko hata ilivyokuwa wakati wa ukoloni au enzi za utawala wa udikteta,” alisema Lutembeka.

Alisema watawala wana hofu ya kuhojiwa na wananchi, wengine hawapo tayari kukubali fikra mbadala  na  mazingira ya aina hiyo ni hatari kwa ustawi wa taifa.

“Sheria zinazominya uhuru wa habari na kukandamiza upatikanaji wa taarifa  sharti zifanyiwe marekebisho.

“Zipo sheria mbovu kama vile sheria ya magazeti, sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mitandao ambazo zote zinaminya uhuru na haki ya kupata taarifa,” alisema Lutembeka.

Wazee hao walionya kuzuiwa kwa vyombo vya habari kurusha matangazo ya bunge moja kwa moja (live) na kusema hivyo ni viashiria vya taifa kurudi nyuma kuliko hata zama za ukoloni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles