32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

UHURU, RAILA WASAKA KURA DAKIKA ZA MWISHO

MOMBASA, KENYA

RAIS Uhuru Kenyatta na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga, jana walikuwa na mikutano ya kampeni ya dakika za mwisho, siku tano kabla ya Uchaguzi Mkuu Jumanne wiki ijayo.

Wakati Rais Uhuru akizuru kaunti za Kilifi na Mombasa baada ya kuzuru Kaunti ya Makueni, mashariki mwa nchi, Raila atarudi katika Bonde la Ufa katika kaunti za Kericho na Narok.

Uhuru analenga kuongeza kura ili atetee kiti chake cha urais katika kaunti hizo tatu zinazohesabiwa kama ngome ya muungano wa upinzani wa Nasa.

Kwa mujibu wa utafiti mpya wa maoni ulioendeshwa na Taasisi ya Infotrak Research and Consulting, Rais Uhuru ana asilimia 32 za umaarufu katika kaunti za Pwani na asilimia 47 katika kaunti za Mashariki, ikiwamo Makueni.

Rais Uhuru ambaye kura za maoni za taasisi hiyo zilionyesha angepata asilimia 48 ya kura nyuma ya Raila mwenye asilimia 49 kwa nchi nzima, alianza kampeni huko Wote, Kaunti ya Makueni, ambayo ni ngome ya Kalonzo Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Raila.

Mpinzani wake Raila amelenga kumharibia mafanikio aliyopata Uhuru wakati alipozuru kaunti za Kericho na Nandi.

Raila alihutubia mkutano katika uwanja wa soka wa Kapkatet, Kericho, ambako vinara wa Jubilee waliweka kambi Jumapili na kisha akaelekea viwanja vya Suswa, Kaunti ya Narok.

Rais Uhuru pia alikuwa Narok Jumapili.

Raila anamtumia Gavana wa Bomet, Isaac Ruto wa Chama Cha Mashinani (CCM), kujaribu kurudisha uungwaji mkono kutoka Rift Valley alioupata mwaka 2007.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles