28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

GGM INAVYOTIMIZA NDOTO ZA WAKULIMA

 

Na Mwandishi Wetu

KATIKA jitihada za kuwezesha wajasiriamali na wakulima mkoani Geita, mgodi wa dhahabu Geita (GGML), umetumia zaidi ya Sh milioni 330 kujenga ghala la kisasa lenye uwezo wa  kuhifadhi tani 30,000 ili kuwezesha wakulima kuhifadhi zao la mpunga.

Hii yote ni moja ya sehemu ya jitihada za GGML kunufaisha jamii inayowazunguka kupitia Mpango wa Maendeleo ya Uchumi Mkoa wa Geita (Geita Economic Development Project – GEDP). Mpango huo unahusisha pia kilimo cha alizeti, ushonaji nguo na kudarizi, uchomeleaji (welding), utengenezaji viatu (shoe making) na ufyatuaji tofali za kisasa (Interlocking blocks), unalenga kuwezesha wananchi kiuchumi.

Tatizo la kuharibika mazao kwa kukosa soko au kuuza bei ya chini ili yasiharibike, imekuwa ni changamoto kubwa kwa wakulima Tanzania na hata Mkoa wa Geita.

Ujenzi wa ghala hilo, unakwenda sambamba na uwezeshwaji wa wakulima kupata mavuno kwa wingi zaidi ya awali, baada ya GGM kupeleka watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya Kilimo CHOLIMA ya mkoani Morogoro na kuwapatia elimu ya ukulima wa kisasa.

Wakulima walikuwa wanavuna magunia tisa kwa heka, lakini sasa wanavuna 35 – 40 kwa heka, imekuwa lazima kuwezesha mfumo mzima wa zao ili kunufaisha wananchi.

Akizungumzia ghala hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Saragulwa na kiongozi wa Chama cha Ushirika kinachojumuisha vijiji vya Nyansalwa, Bugulula, Salagulwa, Kasota na Manga (NYABUSAKAMA Agriculture Marketing Cooperative Society Ltd), Yuda Ng’hindi, anasema ghala hilo ni msaada mkubwa kwa wakulima.

“Tunaishukuru Kampuni ya Geita Gold Mine Ltd kutujengea ghala kubwa la kisasa. Kukamilika kwake ni msaada mkubwa, tunakuwa na uhakika wa kuhifadhi mavuno yetu na kuyauza kwa wakati mwafaka,” alisema Ng’hindi.

Naye Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano wa GGML, Tenga B. Tenga, amesema kampuni yake itaendelea kusaidia miradi endelevu yenye kuleta tija kwa jamii ya Geita na Tanzania kwa ujumla.

“Mradi huu, ni mojawapo tu ya juhudi kubwa tunayoifanya ili kuleta tija kwa wakulima na wakazi wa mkoa huu. GGM itaendelea kuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa wadau na kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania,” anasema Tenga.

Anasema ghala hilo, Kampuni ya GGML pia imewezesha ulimaji wa heka 900, upandaji na ununuzi wa mbolea. Hii ni pamoja na ununuzi wa trekta jipya na kupeleka wataalamu wa kilimo ili kutekeleza kilimo cha kisasa kitakachokuwa na manufaa hata baada ya kampuni ikapomaliza shughuli zake mkoani Geita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles