27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ugonjwa wa Dengue waibukia Bungeni

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

Mbunge wa Viti Maalum Amina Molel (CCM), ameomba muongozo bungeni akitaka Serikali impe majibu ni kwanini imekaa kimya  wakati ugonjwa wa Dengue ukiendelea  kuuwa watu wengi Jijini Dar es salaam.

Akiomba muongozo huo bungeni leo Juni 17 mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Molel amesema kwamba ugonjwa huo umekuwa ni tishio kwa sasa na kwamba taarifa zilizopo watu wengi wamefariki na Serikali imekaa kimya.  

“Mheshimiwa Naibu Spika naomba nizungumzie tatizo lilopo Jijini Dar es salaam hasa ugonjwa wa Dengue, ugonjwa huu umekuwa ni tishio kwa sasa na taarifa zilizopo watu wamefariki wengi na hakuna taarifa sahihi,” amesema.

“Serikali imekuwa kimya juu ya ugonjwa huu na wanapoenda hospital wanaambiwa kipimo ni shilingi 50,000  kwa hiyo watu wengi wanakwepa kupima sababu ya kiasi hicho cha fedha Kwa hiyo Mheshimiwa Naibu Spika  ninaomba ikikupendeza kutumia kanuni ya 49 (1) (2) ili tuweze angalau tupate taarifa ama majibu kutoka kwa Serikali,” amesema.

Akijibu, Naibu Spika Dk.Tulia Ackson amesema suala hilo Serikali imeshalitolea kauli mbalimbali.   

“Waheshimiwa Wabunge ugonjwa alioutaja Mheshimiwa Amina Molel wa Dengue nadhani Serikali imeshatoa kauli mbalimbali katika vyombo mbalimbali hivyo utaratibu wa bei za vipimo hauwezi kujadiliwa humu ndani kwa sababu haijaletwa hoja mahususi kuhusu jambo hilo sasa tukisema tunaanza kujadili bei za vipimo wengine kwao bei kubwa ni CT Scan.

“Hata hivyo hilo jambo pamoja na mambo mengine linatusumbua kwa sasa ila sio jambo la dharura kwa sababu lipo na Serikali imeishatoa taarifa kwa maana hiyo matumizi ya kanuni ya 49 mimi naweza kusema kwamba kwa sababu hii inahusu kauli za Mawaziri,” amesema.

“Serikali ikiona kuna taarifa za ziada ambayo haijatoa mpaka sasa yenyewe itaomba kibali ili iweze kutoa kauli hiyo hapa bungeni kwa kutumia kanuni hiyo lakini kiti hakiwezi kutoa muongozo kwa sababu imeshatoa maelezo ya ugonjwa huo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles