24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yazindua kampeni kwa kishindo Morogoro

Na MWANDISHI WETU -MORORGORO

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, kimewasha moto kwa kuzindua kampeni ya ‘Tuwe pamoja tusikubali kugawanyika’ kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika Oktoba, na Uchaguzi Mkuu mwakani.

Kampeni hiyo ilizinduliwa juzi Uwanja wa Jamhuri mjini hapa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo aliyemwakilisha Katibu Mkuu, Dk. Bashiru Ally.

Mpogolo alisema mgawanyiko na makundi ndani ya chama kwa sasa havina nafasi na kuwaonya wale watakaoanza kufanya hivyo, chama kitawamulika na kuwachukulia hatua za kinidhamu.

“CCM Morogoro iko imara, na sasa itakuwa ya kijani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, ni lazima tushikamane.

“Na yule ambaye sasa anataka kuanza kuleta siasa za makundi ndani ya chama, aanze kuacha mara moja. CCM ni taasisi kubwa iliyoaminiwa na Watanzania chini ya jemedari wetu, Rais Dk. John Magufuli ambaye sasa anafanya kazi kubwa na kila Mtanzania anashuhudia,” alisema Mpogolo.

Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Stephen Kebwe, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani sambamba na ujenzi wa miradi mipya mkoani hapa.

Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, alisema  hatua ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo, inatokana na misingi iliyowekwa na chama, ikiwamo kuimarisha umoja na mshikamano kwa wana CCM wote.

“Tarehe 4 Februari  2019 wakati wa  miaka 42, kule Mikumi tulitangaza kampeni hii ya Morogoro ya Kijani. Tuwe pamoja, tusikubali kugawanyika, tokea kipindi hicho kazi imefanyika,  hata tufanye uchaguzi kesho Morogoro tuko tayari na tutashinda kwa kishindo kuanzia 2019/20.

“CCM ni chama kinachojiamini kisiasa, chama chetu kina sera, na kinajivunia utekelezaji bora wa sera zake. Kiongozi asiyetaka kutoka jasho la kusaka ushindani wa kisiasa ruksa akacheze Baikoko (ngoma),” alisema Shaka.

Katika uzinduzi huo, Mpogolo alipokea wanachama,  madiwani, wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali waliotoka vyama vya upinzani na kujiunga CCM.  

Wanachama hao ni kutoka Chama cha Wananchi (CUF)  3,217, Chadema – 12,547,  ACT-Wazalendo 508 na TLP 198 na kufanya jumla ya 16,470.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles