23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Mahakama yaamuru Wema kwenda Segerea siku saba

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MSANII wa Filamu nchini, Wema Sepetu ameamuriwa kwenda gerezani kwa siku zaidi ya saba hadi atakaporudi kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kumfutia dhamana ama la.

Mahakama imeamuru Wema aende gerezani mpaka Juni 24 mwaka huu , Mahakama itakapotoa uamuzi wa kufuta dhamana yake.

Uamuzi huo wa Mahakama umefikiwa leo Juni 17,  mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wakati mshtakiwa huyo alipofikishwa mbele yake.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.

Wakili wa Serikali Glory Mwenda amedai mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa hapo baada ya mahakama wiki iliyopita kutoa hati  ya kumkamata Wema kwa kosa la kuruka dhamana.

Hakimu Kasonde alimtaka Wema kujieleza kwanini asifutiwe dhamana kwa kushindwa kufika mahakamani kwa tarehe mbili tofauti.

Akijieleza Wema alidai Mei 14 mwaka huu hakufika sababu alikuwa safarini mkoani  Morogoro na Juni 11 mwaka huu aliumwa akashindwa kupandisha mahakamani.

Mshtakiwa aliomba msamaha na Wakili wa Serikali, Mwenda aliomba Mahakama impe onyo mshtakiwa ili asirudie kufanya kitendo hicho chenye usumbufu.

Hakimu Maira alisema kasikia hoja zilizowasilishwa na atapitia kiapo cha mshtakiwa kisha atatoa uamuzi Juni 24 mwaka huu na akaamuru katika kipindi cha kusubiri uamuzi mshtakiwa akae rumande.

Wema anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono katika mtandao wa kijamii.

Wema anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa hazina maudhui.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles