31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ufanisi Bandari ya Dar es Salaam

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imesema maboresho makubwa wanayoendelea kufanyika yataiwezesha kuongoza kwa kuwa bandari kubwa inayopokea magari mengi Afrika Mashariki hadi Kusini mwa Afrika.

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Deusdedit Kakoko, amesema mwaka 2016/2017 walikuwa wakipokea magari 47,000 na sasa wana uwezo wa kupokea na kuhudumia magari 170,000 na magati yanayoendelea kujengwa yatawawezesha kupokea hadi 200,000.

Kwa mujibu wa Kakoko gati namba moja hadi nne ambayo yamekuwa yakitumika, yamewasaidia kupokea meli kubwa za bahari kuu za kimataifa tofauti na ilivyokuwa kabla ya ujenzi.

“Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa meli kubwa za bahari kuu zinapungua kwa idadi, lakini zinaongezeka kwa ukubwa na uwezo tofauti na ndogo zilizokuwa zinakuja kwa wingi,” amesema Mhandisi Kakoko.
Zaidi tazama (Infographics yetu)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles