27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

UCHAGUZI TFF

 

 

 

Katika uchaguzi wa mwaka huu kama zilivyo chaguzi nyingine, zilitokea changamoto mbalimbali, ikiwamo mapingamizi ambapo mmoja wa waliokumbwa na hali hiyo ni mgombea wa nafasi ya urais, Karia, ambaye awali ilidaiwa si raia wa Tanzania, mpaka pale Idara ya Uhamiaji ilipothibitisha uraia wake.

Katika uchaguzi huo, jina la Malinzi halitaonekana, kwani licha ya kwamba alichukua fomu ya kutetea kiti chake hicho, mambo yalimwendea ndivyo sivyo baada ya kushikiliwa na Takukuru na baadaye kupandishwa kizimbani kwa madai ya utakatishaji wa fedha.

Mbali na Malinzi, mwingine ni Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, ambaye naye alichukua fomu akitaka kugombea nafasi ya umakamu wa rais wa TFF, lakini naye mpaka sasa yupo mahabusu kwa madai hayohayo ya utakatishaji wa fedha.

Kutokana na madai hayo, kamati ya uchaguzi ya shirikisho hilo iliamua kuengua majina yao, hasa baada ya kushindwa kufika siku ya usaili kamati hiyo ilipohakiki majina na vyeti vya wagombea.

Mjini Dodoma wajumbe wa mkutano mkuu wamekuwa wakipigana vikumbo, mbali na wajumbe wa mkutano huo, pia wapambe wa wagombea hao wako mjini humo kila mmoja akimnadi mgombea wake

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles