24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MALINZI NA WENZAKE BADO KIZA

 

 

PATRICIA KIMELEMETA NA MANENO SELANYIKA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa Jamhuri kukamilisha upelelezi katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa Shirikisho la na wenzake wawili.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri, amesema hayo jana, baada ya Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Nehemiah Nkoko, aliuomba upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi kwa madai kuwa anaamini upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, lakini  upande wa mashtaka unachelewesha.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa Shirikisho hilo, Nsiande Mwanga.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 28, likiwamo la utakatishaji fedha ambazo ni dola za Marekani 375,418.

Wanadaiwa kuwa, Juni 5, mwaka jana, maeneo ya jiji la Dar es Salaam, Malinzi na Selestine walighushi nyaraka ya maazimio ya kamati tendaji ya Juni 5, mwaka jana kwa lengo la kuonesha kuwa kamati hiyo ya TFF imelenga kubadili mtia saini wa shirikisho hilo katika akaunti za benki kutoka Edgar Masoud kwenda kwa Mwanga.

Inadaiwa Septemba Mosi, mwaka jana, katika benki ya Stanbic iliyopo Kinondoni, Dar es Salaam, Selestine alitoa nyaraka hizo zilizoghushiwa Juni 5, mwaka jana, kuonesha kuwa TFF imebadilisha mtia saini wa akaunti zake za benki kutoka Masoud kwenda kwa Mwanga, kitu ambacho alijua si kweli.

Pia inadaiwa washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa Septemba Mosi na Oktoba 19 mwaka jana, maeneo ya jiji hilo, walitakatisha fedha ambazo ni Dola za Marekani 375,418, huku wakijua kwamba fedha hizo ni zao la kughushi.

Hata hivyo, Malinzi na Selestine wanadaiwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19, mwaka jana, maeneo ya Benki ya Stanbic Kinondoni, walighushi Dola za Marekani 375,418.

Kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19, mwaka jana, katika ofisi za TFF, Mwanga aliwasaidia Malinzi na Selestine kuchukua fedha hizo kutoka Benki ya Stanbic, huku akijua kwamba fedha hizo zimetokana na kughushiwa kwa fomu ya kuchukulia fedha ya Machi 15, mwaka jana.

 

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles