28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KIFAA CHA KAIZER CHIEFS CHATUA SINGIDA UNITED

 

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

TIMU ya Singida United, imeendelea kujiimarisha baada ya kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa kati kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Michelle Katsvairo kwa ajili ya kuitumia katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ujio wa Katsvairo atakayeitumikia kwa mwaka mmoja umekamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni, ambapo wengine ni Elisha Muroiwa, Tafadwaza Kutinyu na Simbarashe Nhivi wote kutoka Zimbabwe pamoja na Shafik Batambuza wa Uganda na Danny Usengimana kutoka Rwanda na Michael Rusheshangoga.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Patrick Sanga, alisema wamemchukua mchezaji huyo kwa mkopo wa mwaka mmoja  akitoke Kaizer Chief.

“Katsvairo anakuwa ni mchezaji wa saba wa kigeni baada ya kuachana na Wisdom Mtasa, aliyetimkia Stand United, hivyo tunaamini ataisaidia timu yetu na kutuletea matokeo mazuri,” alisema.

Alisema mchezaji huyo aliwasili jana hivyo ataenda kuungana na wachezaji wenzake moja kwa moja na kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles