24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Uchaguzi kamati ya Olimpiki Tanzania kufanyika Desemba

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (2025 – 2028) wanatarajiwa kupatikana Desemba 14 mwaka huu katika uchaguzi utakaofanyika jijini Dodoma.

Akizungumza leo Novemba 4,2024 Mwenyekiti wa Kamisheni inayosimamia uchaguzi huo Ibrahim Mkwawa, amesema wamejiandaa vizuri na kusisitiza Watanzania wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali.

Amesema nafasi zinazogombewa ni Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Makamu wa Rais, wajumbe 10 wa kamati ya utendaji ambapo watano watatoka Tanzania Bara na watano Zanzibar.

Aidha amesema nafasi za katibu na mweka hazina sasa zitakuwa za kuajiriwa kutokana na mabadiliko yaliyofanywa kwenye katiba.

“Tumejiandaa vizuri tunawaomba Watanzania wenye nia ya kugombea nafasi hizi wajitokeze,” amesema Mkwawa.

Amesema fomu zitaanza kutolewa kesho ambapo kwa nafasi ya urais na makamu wa rais gharama ya fomu ni Sh 500,000 na kwa wajumbe wa kamati ya utendaji ni Sh 200,000.

Naye Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, amesema kamati itakayochaguliwa itakuwa tofauti kutokana na maboresho ya katiba yaliyofanyika mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles