26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ubalozi wa Tanzania Nigeria waipaisha The Royal Tour katika soko la utalii la Nigeria, Afrika Magharibi

Na Mwandishi Maalumu, Lagos-Nigeria

UBALOZI wa Tanzania, nchini Nigeria umeendelea na mkakati wa kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya ‘Tanzania The Royal Tour’.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kutangaza Tanzania kupitia sekta ya utalii nchini.

Hayo yamethibitika Oktoba 3, mwaka huu, baada ya Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, ulipoandaa onesho maalimu ya filamu hiyo kwa wadau wa utalii wa nchi za Uwakilishi za kituo hicho.

Maonesho hayo yalifanyika sambamba na maonesho ya Utalii ya 18 ya Akwaba, jijini Lagos, Nigeria, ambapo zaidi ya washiriki 500 walishiriki maonesho hayo, na makampuni 30 yalikuwa yakionesha bidhaa zake za utalii vikiwemo vivutio vya utalii wa matibabu.

Aidha, Makampuni matano ya Utalii kutoka Tanzania yalishiriki na kupata fursa ya kukutana na wadau wa utalii wa soko la Afrika Magharibi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles