22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

MSCL yaanza ukarabati wa MV Liemba

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Kampuni ya huduma za meli Tanzania (MSCL) imeanza ukarabati wa meli kongwe ya Mv Liemba yenye umri wa miaka 105 ambayo ilikuwa haifanyi kazi kwa muda mrefu.

Hayo yameelezwa leo Novemba 1,2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya huduma za meli (MSCL), Eric Hamis wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji na mwelekeo wa bajeti ya Kampuni hiyo kwa mwaka wa Fedha 2022/23.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya huduma za meli (MSCL) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma

Hamis amesema ukarabati wa meli hiyo utagharimu Sh bilioni 16 mpaka kukamilika kwake ambapo sasahivi Sh bilioni 8.1 zimetolewa kwa mwaka wa Fedha 2021/22 kwa awamu ya kwanza.

“Ukarabati wa meli hii utasaidia kuongeza kasi ya utoaji huduma kwani inaweza kubeba abiria 600 na tani 200 za mizigo, itakapokuja meli mpya na hii ikikamilika itaondoa kabisa changamoto ya usafiri Ziwa Tanganyika,” amesema Hamis.

Aidha Eric amesema Kampuni pia inafanya ukarabati wa meli ndogo ya Mv Muongozo ambayo iliharibika miaka mingi iliyopita ambapo tayari Sh bilioni 1 imetengwa mwaka 2022.

Aidha katika mradi mwingine Kampuni imefanikiwa kujenga chelezo kubwa Ziwa Tanganyika itakayotumika kwenye ujenzi na ukarabati wa meli ambapo itakuwa na uwezo wa kubeba meli yenye tani 5,000 .

Amesema mradi huo utakaogharimu Sh bilioni 50 tayari umetengewa Sh bilioni 12 mwaka huu na utakamilika ndani ya kipindi cha miezi 14.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles