LAGOS, NIGERIA
United Bank of Africa (UBA) imeadhimisha miaka 70 tangu ilipoanza kutoa huduma za kibenki kwa wateja wake wakati.
Katika sherehe za maazimisho hayo zimeudhuriwa na wateja, wafanyakazi na watu wa karibu wa benki hiyo pia zoezi la utoaji tuzo za kila mwaka zilitolewa kwa wafanyakazi kutoka nchi zote 23 ambako benki hiyo inaendesha shughuli zake.
Miongoni mwa watu mashuhuhuri waliohudhulia usiku huo ni viongozi wa dini, viongozi wa zamani na wasasa wa majimbo mbalimbali nchini Nigeria.
Aidha rais wa zamani, Olusegun Obasanjo na Ibrahim Babanginda, walioshindwa kuhudhuria hafla hiyo kupitia ujumbe wa barua waliotuma wameipongeza benki hiyo kwa ufanisi na mafanikio makubwa wanayoyapata.
Mwenyekiti wa benki hiyo, Tony Elumelu, ambaye aliambatana na mkewe, Dk Awele, amesema benki yao ndiyo taasisi ya kifedha pekee inayoongoza barani Afrika na kutimiza kwake miaka 70 ni mafanikio makubwa kwao na wateja wao.
Amesema, “Huu ni wakati wa kusherehekea urithi tajiri wa kipindi cha miaka mingi na kumwambia kila mtu aliyechangia kile kinachoifanya UBA isimame imara leo hii.”
Viongozi wengine waliotoa pongezi zao ni mkurugenzi mtendaji, Kennedy Uzoka na mwenyekiti wa benki ya Zenith, Jim Ovia.
Ovia amesema; “UBA inabakia kuwa moja ya benki kubwa kabisa. Najuta kutonunua hisa za UBA, lakini nadhani sijachelewa kufanya hivyo”.